Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk Jakaya Kikwete anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya Siku ya Albino kitaifa yatayofanyika
Juni 13,mwaka huu kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake leo,Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Felix
Ntibenda alisema wamepata fursa ya kuwa wenyeji kutokana na kutokua na
matukio ya ukatili wa watu wenye ulemavu wa ngozi kutokana na takwimu za
mkoa wapo Albino 199.
“Mkoa
una jumla ya watu wenye ulemavu wa ngozi wapatao 199,wakiwemo
wananwake 110 na wanaume 89,hadi sasa hakuna kitendo chochote cha
kikatili kilichowahi kutokea kwa Albino yeyote hapa mkoani na hivyo
kuipa sifa mkoa wetu kuwa mwenyeji wa maadhimisho haya,”alisema Ntibenda
Hata
hivyo alikiri kuwa taswira na ramani ya nchi imetiwa doa kimataifa
kutokana na mauaji yanayoendelea katika mikoa mbalimbali nchini
inakadiriwa watu wenye ulemavu wa ngozi 74 wameuawa na watu wenye imani
potofu za kutumia viungo vyao kupata utajiri na mvuto kisiasa.
Ntibenda
alisema jumla ya Albino 59 wamenusurika vifo huku 11 wakipewa ulemavu
wa kudumu jambo ambalo serikali ikishirikiana na wadau wengine wameamua
kusimama pamoja kupinga mauaji ya kinyama kwani kila mtu kila mtu ana
haki ya kuishi.
No comments:
Post a Comment