Mamia ya wananchi wakimsikiliza mbunge Joshua Nassar wakati akizungumza katika mkutano huo. |
Mbunge Joshua Nassar alitumia pia mkutano huo ,kukabidhi magari mawili ya kubebea wagonjwa katika jimbo la Arumeru Mashariki. |
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii KAnda ya Kaskazini.
WANANCHI
wa vijiji vya Leguruki na King’ori katika wilaya ya Arumeru wameandaa
sherehe kubwa kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua
Nassar baada ya kutatua mgogoro wa maji uliodumu kwa muda mrefu katika
vijiji 15 vya wilaya hiyo.
Sherehe
hiyo iliyoenda sanjari na shughuli za kimila ilishuhudiwa mbunge huyo
pamoja na mkewe Anande Nnko wakivishwa maazi ya kimila pamoja na
kukabidhiwa rungu huku mkewe akikabidhiwa kibuyu pamoja na ijiti cha
kimila.
Uamuzi
wa wananchi hao unatokana na Mbunge Joshua Nassar kutatua mgogoro kwa
kuunda timu ya viongozi wa Din,Mila,Vijiji na kuamua kuwapeleka Dodoma
na kukutana na Waziri wa maji,Waziri wa Tamisemi na Waziri wa Nishati na
Madini kwa ajili ya mazungumzo.
Safari
ya viongozi hao ndio iliyozaa kuvunjwa kwa iliyojiita bodi ya maji
yaliyofadhiliwa na shirika la OIKOS East Africa kwa vijiji 15 katika
wilaya hiyo huku ikiwalipisha wananchi kwa lita.
Mbali
na kutozwa fedha kwa wananchi hayo bodi hiyo pia ilidaiwa kusababisha
baadhi ya wananchi kuwekwa rumande kwa hila huku mbunge huyo akipambana
na kufanikiwa kuwatoa.
Katika
sherehe hiyo viongozi wa mila na dini walimsimika Nassar huku wakiahidi
kuendelea kumuunga mkno katika mapambano ya kupigania wananchi wa Meru
ili kuondokana na hali ya umaskini.
Akizungumza
katika hotuba yake ,Nassar alisema bodi ya maji imevunjwa na kauli ya
waziri wa maji ni "wananchi ndio wenye Mamlaka ya mwisho kimaamuzi.
“Linapokuja
swala la namna bora ya kuchangia na sio kulipia, ikizingatiwa mradi huu
ulijengwa kwa nguvu za wananchi bila malipo yeyote kwa miaka 3 wananchi
wanapaswa kupata huduma hii ya maji”alisema Nassar.
Nassar
alitumia sherehe hiyo kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa huku
yakiombewa na kuwekwa wakfu ili yakawe sehemu ya uponyaji kwa watu wa
Arumeru Mashariki.
Wananchi wamekiri kwa umoja wao "hawajawahi kupata Mbunge Kama Nassari baada ya Japhet Kirilo.
No comments:
Post a Comment