WAZIRI MKUU
Mizengo Pinda ambaye pia ametangaza nia ya kuwania urais wa Tanzania kwa
tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) amepata wadhamini 1,897 katika
wilaya tatu za mkoa wa Rukwa. Akitangaza idadi ya watu walijitokeza
kumdhamini Waziri Mkuu, Katibu wa CCM wilaya ya Sumbawanga Vijijini,
Bibi Lucy Mfupe alisema wadhaminini wote hao wametoka katika wilaya tatu
za Nkasi, Sumbawanga Mjini na Sumbawanga Vijijini.
Alisema
katika wilaya ya Nkasi, Waziri Mkuu Pinda amepata wadhamini 1,627 wakati
katika wilaya mbili za Sumbawanga Mjini na Vijijini amepata wadhamini
270Mapema leo asubuhi, Waziri Mkuu alipita katika ofisi ya CCM Wilaya
ya Nkasi na kuwashukuru wananchama wote waliomdhamini. Mchana
alifika ofisi ya CCM wilaya ya Sumbawanga Mjini na kutoa shukrani
kwa wadhamini waliokuwa wamefika kwenye ofisi hizo.
Akitoa nasaha
zake kwa wakazi hao, Waziri Mkuu aliwashukuru wote waliomdhamini huku
akiwaomba waendelee kumuomba Mungu ili aipatie nchi hii kiongozi
mwadilifu na mpenda watu na hasa watu wenye hali ya
chini. Alisema ana imani kuwa Chama cha Mapinduzi kitampitisha
kiongozi mwenye kutetea maslahi ya wanyonge ili wapate fursa ya kusonga
mbele zaidi. Mchana huu anaelekea Mbozi na Mbeya Mjini.
IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JUNI 16, 2015.
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, JUNI 16, 2015.
No comments:
Post a Comment