Hii
ilikuwa tarehe 15.06.2015 ambapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Mh. Abbas
Kandoro aliwaaga rasmi vijana hao ili kuanza safari yao kutoka Mbeya
kwenda Dar.
Safari
yao ikiwa imeanza na hapa mmoja wa vijana hao wakiwa safarini na hapa
akonesha umahili wa utaalam wa kuchezea Baiskeri Maeneo ya Chimala
Tarehe 17.06.2015 wanawasili Iringa na kulala Hapo kisha asubuhi wanaonana na uongozi wa Polisi Mkoani Iringa
vijana
hawa watatu wakiwa Iringa sasa wanahimiza watu kujiandikisha katika
Daftari la kudumu la kupigia Kura, na hapa wanadhihirisha kuwa wao
wanavyo tayari, je wewe umeijiandikisha?
Tarehe
18.06.2015 vijana hawa wanaendelea na safari yao ya kutoka Mbeya
kuelekea Dar es salaam na hapa wanaanza kushuka mlima Kitonga ambapo
wanaenda kulala Mikumi.
Hapa wanapumzika maeneo ya kati kati ya Mlima Kitonga
Sasa wanapata chakula Baada ya kumaliza kushuka mlima kitonga
Usiku wa Tarehe 18.06.2015 wakiwa Mikumi
Haya yalikuwa ni baadhi ya Mataili ambayo walibadilisha wakiwa mikumi
Ni
Tarehe 19.06.2015 asubuhi na mapema vijana hao wakiwa wameaka ili
kuzirekebisha Baiskeli zao tayari kwa kuvuka Hifadhi ya Taifa ya
Mikumi.
Tarehe
19.06.2015 vijana hao watatu wakiwa na Baiskeri zao sasa wanajiandaa na
kuanza kuvuka Hifadhi ya Taifa ya Mikumi ambapo walitembea kwa Kilometa
50
Wakiwa ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi
Mmoja wa vijana hao akiwa anatazama ndani ya Hifadhi kama ataona wanyama
Wakiendelea na Safari yao
Wakimalizia malizia safari yao ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Mikumi.
Leo Tarehe 20.06.2014 vijana hawa wanaondoka Morogoro kuendelea na safari na hapa wakiwa wameweka Hema lao Mjini Morogoro.
Vijana
hawa watatu ambao ni Wise Man Tanzania,John Mwaipaya na Alex Mahenge
walioamua kusafiri kwa kuendesha Baiskeri kutoka Mbeya mjini hadi Dar es
salaam kwa lengo la Kuhamasisha watu kujiandikisha katika Daftari la
kudumu la kupiga kura na Baadae wakifika Jijini Dar kwa lengo la
Kumpongeza Rais Dkt. Jakaya Kikwete kwa uongozi wake Bora katika kipindi
cha Miaka 10 akiwa ameshika wadhifa wa Kiongozi Mkuu wa nchi.
Vijana hao ambao wameanza safari Tarehe 15.06.2015 wakitokea Mbeya sasa wapo Morogoro wanaendelea na Safari.
No comments:
Post a Comment