Mwenyekiti wa CCM
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu Mwenyekiti Zanzibar ambaye pia ni Rais
wa Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein(kushoto), Makamu Mwenyekiti Bara Ndugu Philip
Mangula(kulia) na katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana(watatu kushoto) wakati
ufunguzi wa Kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM kinachofanyika
katika ukumbi wa White House Mjini Dodoma.
***********
Kamati Kuu imepokea na kutafakari taarifa ya Kamati ya Usalama na
Maadili ambayo ilipitia adhabu waliyopewa wanachama sita waliokiuka
kanuni za Maadili na kupewa Onyo Kali, adhabu iliyodumu kwa kipindi
kisichopungua miezi 12.
Wanachama hao sita ni;-
i. January Makamba
ii. Willium Ngeleja
iii. Steven Wasira
iv. Bernard Membe
v. Edward Lowassa
vi. Fredrick Sumaye
Kamati Kuu imepokea na kukubali pendekezo la Kamati ya Usalama na Maadili ya kumalizaka kwa kipindi cha adhabu kwa wanachama hawa. Kwahiyo adhabu hiyo kwa sasa imemalizika, na wanachama hao wameruhusiwa kuendelea na shughuli zao katika Chama.
Hata hivyo Kamati Kuu inawataka wanachama hawa na wale wengine wenye nia ya kugombea Urais kupitia CCM Kuzisoma , Kuziheshimu na Kuzizingatia Kanuni za Maadili za CCM na kanuni zingine zinazoongoza mchakato ndani ya Chama, ili wasikumbwe na adhabu itokanayo na kuzivunja kanuni hizo.
Wale wote wanaotaka kugombea, yaani waliokuwa kwenye adhabu na wengine watakaojiingiza kwenye kampeni mapema na hivyo kukiuka maadili na miiko ya Chama, taarifa za kukiuka kwao zitatumiwa wakati wa kuchuja majina ya wagombea utakapofika.
Taarifa hizo zitatumika katika kuwapima na kuamua iwapo wana sifa za kutosha na wanafaa au hawafai katika kupata uteuzi wa nafasi wanayoiomba.

Katibu
wa NEC Uchumi na Fedha Mhe. Zakhia Meghji akizungumza na Katibu wa NEC
Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro kwenye ukumbi wa NEC
mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa Kikao cha Kamati Kuu leo tarehe 22 Mei
2015 mjini Dodoma.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe.Jerry Slaa akishauriana jambo na Mhe.Wiliam Lukuvi ndani ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na
Wajumbe wenzake wa Kamati Kuu Profesa Makame Mbarawa Mnya na Dk. Salim
Ahmed Salim kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma wakijiandaa na kikao cha
Kamati mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezu Nape Nnauye akisoma gazeti ndani ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati Kuu Dk. Emmanuel Nchimbi akizungumza na wajumbe wengine
Abdala Bulembo na Hadija Aboud ikiwa sehemu ya kujiandaa na kikao cha
Kamati Kuu kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na Profesa Makame Mbarawa Mnya huku Dk.
Salim Ahmed Salim akipitia baadhi ya makabrasha kwenye ukumbi wa NEC mjini Dodoma wakijiandaa na kikao
cha Kamati mjini Dodoma.
Mjumbe
wa Kamati Kuu CCM Taifa Mhe.Adam Kimbisa akimsikiliza kwa makini mjumbe
mwenzake Mhe.Stephen Wasira kabla ya kikao cha Kamati Kuu kuanza ndani
ya ukumbi wa NEC mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment