Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano ambao walitoa tamko la kupinga uongozi wa chama wilaya kuwaburuza kwenye mchakato wa ubunge wilayani humo. |
Arusha.Wanachama wa
Chama Cha Mapinduzi(CCM) wilaya ya Monduli zaidi ya 600 wamewatuhumu viongozi
wa chama hicho kwa kuwaburuza katika maamuzi na kuwaamulia nani atakua mbunge
wa Jimbo hilo baada ya Mbunge wa sasa,Edward Lowassa kutajwa kutogombea nafasi
hiyo.
Wana CCM hao kutoka
Kata zote 20 walidai kumekuwepo na ukiukwaji wa makusudi wa kanuni za chama
unaongozwa na Katibu wa CCM wilaya,Elisante Kimaro kufanya ziara za kichama na mmoja wa
waliotajwa kugombea ubunge jimbo hilo na kumtambulisha kinyume na kanuni za
chama hatua iliyozusha mgogoro na kuhatarisha uhai wa chama.
Katika barua yao kwa Katibu wa CCM mkoa,Alphonce Kinamhala
inawataja moja kwa moja Mjumbe wa kamati ya Siasa ya mkoa,Paulo Kiteleki ambaye
ni Katibu Tarafa ya Kisongo,Mjumbe wa Kamati ya Siasa na maadili wa wilaya ,Kalaine
Lowassa,Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake(UWT)wilaya,Einoti Leringa na Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya ya Monduli,Edward Sapunyu.
Wengine wanaotuhumiwa kukiweka chama rehani kwa maslahi yao
ni Mjumbe wa Kamati ya siasa ya wilaya ambaye pia ni diwani wa Kata ya Monduli
Juu,Bariki Sumuni na Katibu wa Hamasa wa Umoja wa vijana(UvCCM)Kimani
Ndiarakombe.
“Tunaomba viongozi wetu wakumbuke ya kuwa kuwepo CCM ni
kuwepo kwa wanachama ambao haki zao zinaheshimiwa na kupewa demokrasia ndani ya
chama chao na sio viongozi wa ngazi husika wanaamuakwa maslahi yao kukiuka
taratibu za chama kwasababu wamepewa dhamana ya kuwa viongozi.”ilisema sehemu
ya barua hiyo
Hata hivyo Katibu wa CCM wilaya ya Arusha ,Elisante Kimaro alikanusha
taarifa hizo na kudai hazina msingi wowote bali kinachofanyika ni ziara ya kawaida
ya kuwashukuru wananchi kutokana na ushindi mkubwa walioupata kwenye uchaguzi
wa serikali za mitaa mwaka jana ambapo Mbunge wa Viti Maalum,Namelok Sokoine ni
Mjumbe ambaye ametoa mchango mkubwa kwa wanawake na vijana.
Mwakilishi wa Kata ya Lorkisale,Lembrisi Klamian na Parmelo
Ngoyo kutoka Kata ya Sepeko walisema zama za kuburuzwa zimepitwa kila jambo linapaswa kufanyika kwa
ushirikishwaji na sio kuwapandikiza wagombea wao bila ridhaa za wanachama.
Wanachama hao wamesema iwapo malalamiko yao
hayatashughulikiwa ipasavyo na kwa wakati kwasababu wanaolalamikiwa ni wajumbe
wa kamati za maamuzi ngazi ya wilaya na mkoa watalazimika kutafuta njia mbadala
ya kufikisha malalamiko yao kwa uongozi wa ngazi ya taifa.
Wanachama Teshi Oloing’ola kutoka Kata ya Lepurko na Osidai
Nadongala wa Kata ya Mbwakiri walisema kinachowasikitisha ni kuwa wajumbe wa
kamati ya siasa na kamati ya maadili wilaya kwenye kampeni za kumnadi mgombea
anayenadiwa na msimamia taratibu za chama ambaye ni Katibu wa wilaya.
Hata hivyo walidai viongozi hao wa wilaya kutumiwa na mmoja
wa viongozi wakubwa wilayani humo bila kutaja jina .
No comments:
Post a Comment