Kiongozi
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum akiwa ameshika
mwenge baada ya kufika mtaa wa Kisutu jijini Dar kwenye uzinduzi wa
magari mapya ya kuzoa taka katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na na
kampuni ya Green WastePro ltd. Picha na Geofrey Adroph wa Pamoja Blog
Mkuu
wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi akizungumza jambo mara baada ya
Mwenge wa Uhuru kufika eneo la Kisutu jijini Dar kwa ajili ya ufunguzi
wa Magari ya kisasa ya kuzoa taka.
Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum
akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa magari ya kufanyia usafi
yanayomilikiwa na Kampuni ya Green Waste Pro ltd.
Meneja
mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena
akisoma risala kwa mgeni rasmi ambaye ni kiongonzi wa mbio za mwenge wa
uhuru kitaifa mwaka 2015 , Bw. Juma Khatibu Chum (hayupo pichani).
Kiongozi
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (kushoto)
akikabidhiwa risala na Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro
Ltd, Bw.Abdallah Mbena iliyosomwa wakati wa uzinduzi wa magari ya
kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala jijini Dar.
Kiongozi
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum (wa kwanza kushoto),
Mkurugenzi wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo
(katikati) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi wakiwa
kwenye zoezi la kuweka uchafu kwenye moja ya gari la kufanyia usafi
lililozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Mmoja
wa viongozi wa Mbio za Mwenge akizungumza mara baada ya uzinduzi wa
magari ya kufanyia usafi katika manispaa ya Ilala yanayomilikiwa na
Kampuni ya Green Waste Pro Ltd aliwasisitiza wananchi kuendelea kutumia
kampuni hiyo kwani usafi utaendelea kuimarika zaidi na zaidi.
Kiongozi
wa Wakimbiza Mwenge Kitaifa, Bw. Juma Khatibu Chum(wa kwanza kushoto),
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (wa pili kutoka kushoto), Naibu
Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Kheri Kessy(katikati) Mkurugenzi wa Green
WastePro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo( wa pili kutoka kulia) pamoja na
Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw. Abdallah Mbena
wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa magari ya
kufanyia usafi katika eneo la Kisutu jijini Dar.
Mmoja
wa viongozi wa mbio za mwenge akiwa ameshikiria Mwenge wa Uhuru tayari
kwa kuondoka mara baada ya kumaliza uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi
mali ya kampuni ya Green Waste Pro Ltd inayofanya kazi za usafi katika
manispaa ya Ilala jijini Dar.
Mkurugenzi
wa Manispaa ya Ilala Ndugu Isaya M. Mngurumi (kushoto) akimsikiliza
Mkurugenzi wa Green Waste Pro Ltd Ndg. Mark Anthony Shayo akiwa na
Meneja mwendeshaji wa kampuni ya Green Waste Pro Ltd, Bw.Abdallah Mbena
wakiwa wanatoa maelezo juu ya uzoaji na usindikaji wa Taka
zinazokusanywa katika sehemu mbalimbali za Manispaa ya Ilala na jinsi ya
watakavyoyatumia magari hayo yaliyozinduliwa na Mwenge wa Uhuru.
Akizungumza wakati wakati wa tukio
la uzinduzi wa magari ya kufanyia usafi ya Kampuni iliyopewa zabuni
kusafisha manispaa ya Ilala, Green Waste Pro Ltd Mkuu wa Wilaya ya
Ilala, Raymond Mushi amesema kushirikiana vyema kwa kampuni Green Waste
Pro Ltd ndiko kunako pelekea maendeleo na afya bora katika manispaa ya
Ilala hivyo tuwaunge mkono wenzetu kwa kuwapa ushirikiano wa kuto tupa
taka hovyo bali maeneo husika yaliyo wekwa kwaajili ya kuhifadhi taka
hizo ili waweze kuzipitia kwa urahisi na kuzipeleka mahala panapo
husika.
No comments:
Post a Comment