Balozi
wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Flaviana Matata, ambaye ni Mwanamitindo
na Mbunifu Mavazi maarufu nchini Tanzania, kwa sasa akifanyia kazi zake
nchini Marekani, akizungumza wakati wa semina ya siku moja, iliyowaleta
pamoja, wanamitindo "kinda" wa Tanzania, kwenye hoteli ya Serena jijini
Dar es Salaam Jumapili Mei 17, 2015. Semina hiyo ililenga kuwafunza na
kubadilishana uzoefu juu ya tasnia hiyo inayokuwa kwa kasi. Semina hiyo
ya siku moja, ilitayarishwa kwa pamoja na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, na
mwanamitindo huyo nguli. Katika maelezo yake, Flaviana, alisema yeye
binafsi ni mwanachama wa Mfuko huo kupitia mpango wa hiari yaani "PSPF
Supplementary Scheme-kwa kifupi PSS", na kuwataka wanamitindo
waliohudhuria semina hiyo, kufuata nyayo zake. Aliwaeleza umuhimu wa
wanamitindo hao ambao wengi ni vijana, kujiunga na mpango huo kwa faida
yao ya sasa na baadaye, kwani yeye anafaidika sana kuwa mwanachama wa
Mfuko huo. Baada ya maelezo hayo yaliyofuatiwa na balozi mwingine wa
Mfuko huo, Msanii maarufu wa muziki wa majigambo, Mrisho Mpoto, naye
aliwapa "doze" wanamitindo hao juu ya ukuhimu wa wao kuchangamkia fursa
mapema kwani ndio mtindo wa kisasa. Hali kadhalika afisa masoko wa Mfuko
huo Magira Werema, aliwahakikishia wanamitindo hao kuwa Mfuko huo ni
Mfuko bora na wala hawatajuta waingiapo kuwa wanachama. Baada ya hotuba
hizo, wanamitindo hao walizichangamkia fomu za kujiunga na uanachama wa
Mfuko huo amba;po karibu washiriki wote zaidi ya 100 walijiunga na Mfuko
huo. |
No comments:
Post a Comment