
Goodwill Zwelithini, Mflame wa Zulu.

Raia moja wa kigeni akishambuliwa nchini Afrika Kusini.

Mama mmoja raia wa kigeni ambaye nyumba yake ilivamiwa nchini Afrika Kusini
Mfalme wa
kabila la Zulu, Goodwill Zwelithini, ameelezea kama jambo la aibu
mashambulio dhidi ya raia wa mataifa mengine yanayofanyika nchini Afrika
Kusini, ambayo tayari yamesababisha vifo vya watu saba.
Mwaandishi
habari wa BBC mjini Durban mahala ambapo mfalme huyo alitoa matamshi
hayo anasema kuwa hata ingawa anakanusha kuwa amenukuliwa visivyo,
matamshi yake dhidi ya raia wa kigeni imesababisha athari mbaya.
Amesema kuwa umma uliwapigia kelele mabalozi wanaoziwakilisha mataifa yaliyoathirika zikiwezo Msumbiji na Zimbabwe.
Polisi
nchini humo wameakamata washukiwa kadhaa miongoni mwao wanaume watatu
ambao wanatuhumiwa kuhusika na mauaji ya rais mmoja wa Mozambique katika
eneo la Alexandra viungani mwa mji mkuu wa Johannesburg.

Post a Comment