Pages

April 12, 2015

ZIARA YA CHAMA CHA ACT-WAZALENDO NDANI YA NYANDA ZA JUU KUSINI

 Viongozi wa Chama cha ACT –Wazalendo wakiangalia mazao ya wakulima waKijiji cha Mkongotema wilayani Songea vijijini jimbo la Peramiho jana
aliposimamishwa kijijini hapo ili afungue tawi la chama hicho jana.
wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe wakifuatilia yaliyokuwa yakjiri kwenye mkutano huo wa hadhara jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
 Askari wa jeshi la polisi wakiimarisha ulinzi kwenye mkutano wa chama
cha ACT-Wazalendo mjini Njombe jana.
 Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa Njombe wakifuatilia
kwa makini huku wakinyeshewa na mvua.
  Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
   Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akisalimiana na Wananchi mara baada ya kumaliza wahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
   Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency (ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiondoka mara baada ya kumaliza mkutano wa hadhara ndani ya mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
  Katibu Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Samson Mwigamba akiwahutubia wakazi wa mji wa Makambako mkoani Njombe jana, wakati wa ziara ya chama hicho inayoendelea mikoa ya nyanda za juu kusini.
 Kiongozi wa Chama cha Alliance For Change and Transparency
(ACT-Wazalendo) Zitto Kabwe, akiwahutubia wakazi wa mji wa Njombe huku akinyeshewa na mvua mjni humo jana ambapo wakazi waliojitokeza
walikubali kulowa ili kumsikiliza.



Rais Jakaya Kikwete ametakiwa kuitisha Bunge Maalum haraka
iwezekanavyo ili ili liweze kufanya marekesho madogo ya katika ili
kuruhusu uchaguzi ufanyike kwa uhuru na haki.

Kauli hiyo imetolewa na CHAMA cha Alliance For Change and Transparency
(ACT-Wazalendo), wakati akizungumza kwa nyakati tofauti Mkoani Njombe
na Mji Mdogo wa Makambako wakati wa ziara ya chama hicho ya kuimarisha
chama hicho mikoani.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo,
Anna Mghwira,  alisema sasa umefika wakati ni lazima nchi iwe huru kwa
kuwa na misingi imara itakayoimarisha demokrasia nchini.
“Rais aitishe Bunge maalumu ili kufanya marekebisho madogo ya Katiba
kuruhusu uchaguzi huru na wa haki lakini pia Wajumbe wa Tume waombe
kazi na wawe wataalamu.

“Kwa nini ACT tunashauri kuitwa Bunge Maalumu ni kutokana na uhai wa
Bunge la 10 umebaikisha mkutano mmoja kabla ya kuvunjwa.
“… hivyo Katibu wa Bunge atangaze nafasi za wajumbe wa Tume, kamati ya
Bunge ya Katiba Sheria na Utawala itafanya mahojiano ya wazi na kupata
majina 22 yatakayopelekwa bungeni,” alisema Anna

Alisema baada ya kukamilka kwa mchakato huo huo, Bunge litapiga kura
kuchagua watu 11 ambao majina yao watapelekwa kwa Rais ambaye naye
atawatangaza kuwa makamishna wa Tume huru ya uchaguzi pamoja na
kumteua mwenyekiti kutoka miongoni mwa makamishna hao waliopitishwa na Bunge.

Alisema kutokana na hali hiyo ili kuweza kuwa na tume huru ya
Uchaguzi, Tanzania inaweza kutumia mfumo uliotumiwa na nchi ya
Msumbiji ambayo kila chama kinateua mwakilishi au kufuata utaratibu wa
kutangaza majina kupitia Bunge.

“Kama tukifanikiwa kupata tume huru ni wazi mwaka huu tutakuwa na na
Uchaguzi huru na haki kuliko miaka yote iliyopita,” alisema.

Kwa upande wake Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, alisema
kuporomoka kwa maadili ya Taifa kutokana na kukosekana na viongozi
wanaipinga rushwa kwa vitendo kama ilivyokuwa ikifanywa na Waziri Mkuu wa zamani, Edward Moringe Sokoine.

Kutokana na kukosekana kwa uadilifu kwa viongozi ni wazi sasa Taifa
linashindwa kusukumwa na viongozi waliopo Serikalini na badala yake
wanaimba uadilifu huku wakishindwa kutekeleza kwa vitendo.
“Kesho nchi inakumbuka kifo cha Sokoine, ambaye alifariki Aprili 12,
mwaka 1984 yaani kesho (leo) lakini kifo chake ni wazi kwetu
 
ACT-Wazalendo tunamkumbuka kwa uwajibikaji wake kwa vitendo.
“… leo nchi inayumba ufisadi kila kukicha umekuwa ukitamalaki  jambo
ambalo lilipigwa na Sokoine kwa kuikata rushwa na hata kupinga uhujumu
uchumi kwa makusudi nab ado nchi ilisimama katika uadilifu kama
tunavyoamini ACT,” alisema

Alisema kama Sokoine angakuwa hai hakuna kiongozi wa Chama Cha
Mapinduzi (CCM), ambaye angetembea barabarani na kufanya wanayofanyika
sasa.
 
Azimio la Songea
Alisema akiwa Mbunge aliwasilisha hoja mbalimbali ikiwemo utekelezaji
wa azimio la Songea ambalo lilitaka uwazi na wajibikaji kwa Serikali.
“Nilipokuwa bungeni nilisema kuwa mikataba yote ni lazima iwe wazi
lakini nilikosa kuungwa mkono na wabunge wenzangu na si hilo tu
nilisema mishahara ya ya wabunge ikatwe kodi pia sikuungwa mkono je
kisa langu ni nini.

“Tulishindwa kutekeleza suala la mikataba ya madini ambapo leo hii
wawekezaji wananufaika na madini lakini wananchi wakibaki kuwa
watazamaji jambo hili si jema. Nayi hapa Njombe mna madini  mengi
mengi  kule kwa rafiki yangu Filikunjombe,” alisema.

Zitto alisema si kazi yake kutoa matusi kwani hatua yake ya kuhamia
chama kipya cha ACT-Wazalendo, kusiibue malumbano ila waachiwe
Watanzania ndio waamuzi wa “Leo tumewaleta chama mbacho hamtojutia kwa kuunga mkono kama ikitokea kuwaambia tunakwenda bungeni hatuchukui posho basi hatuchukui kweli
kuliko ilivyo sasa,” alisema

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...