
Amekua akisumbuliwa na tatizo la kutoweza
kushika ujauzito ambapo baada ya ukimya mwingi, Wema ameamua kuongea
yafuatayo kwa wote wanaombeza kutokana na tatizo lenyewe.
Amesema >>> ‘Ningekuwa
na uwezo wa kuzaa ningekuwa nimezaa muda mrefu sana… But sina… Na
siwezi kumkufuru mwenyezi mungu…. Au mngependa niwe nawaambia jinsi
ninavyo hangaika usiku na mchana kupata mtoto wangu mwenyewe… Is dat wat
u want…? kila ntakachofanya kwa ajili ya tumbo langu basi nitangaze… Au
mnadhani siumii mnavyosema kuhusu maswala ya mtoto‘

mnaona nafurahia sio…. hivi mna nini jamani… yaani mtu
unaweza weka post kwa nia nzuri then people jus come from nowea wanaanza
kukuandikia maneno ya kukuumiza kabisa nafsi hadi mtu unakaa unajiuliza
umemkosea nini mwenyezi Mungu‘
‘Kwani kuna
niliemkosea yoyote mpaka muanze tu kunikashif na kunitolea maneno mazito
namna hio… Kisa mtoto… mnadhani naipenda hii hali… hata mimi natamani
kuitwa mama na hakuna kinachoniuma kama hicho…. So mnadhani sijui kama
umri unaenda na maisha yenyewe sikuhizi mafupi anytime we die…
Mnafikiria nisingependa kuacha hata ka copy kangu siku ndo Mungu anasema
ananichukua’
No comments:
Post a Comment