Na Anwar Binde.
Mlinzi wa
pembeni wa Real Madrid Dani Carvajal amekataa tuhuma za kumn’gata
mshambuliaji wa Atletico Madrid Mario Mandzukic wakati wa mchezo wao wa
robo fainali ligi ya mabingwa uliofanyika jana jumanne. Vyombo
mbalimbali wa habari nchini Hispania wanamtuhumu carvajal kumn’gata na
kiwiko halafu kumtandika ngumi maneo ya tumboni ilionyesha kipande cha
video toka Vicente Calderon.
Mandzukic
alihusishwa katika matukio mengi ya vurugu dhidi ya Real,pia
mshambuliaji huyo toka taifa la Croatia pia alipata majanga mengine
baada ya kupigwa kiwiko na mlinzi wa Real Sergio Ramos na kumpasua
sehemu ya puani iliyompelekea kuvuja damu na kupata matibabu.
Lakini
Carvalaj alipinga kufanya tukio hilo,“niliona baada ya mchezo kuisha
kwamba natuhumiwa kumn’gata mpinzani wangu”aliandika kwenye mtandao wake
wa twitter.
Kocha wa
Atletico Diego Simione aliulizwa kuhusu tukio wakati wa mkutano na
waandishi wa habari baada ya mchezo kuisha alisema “sikuliona tukio hilo
na siwezi kusema lolote”.
Kocha
huyo raia wa Argentina mwenye umri wa miaka 44 aliongeza kuwa kiwiko
alichopigwa Mandzukic na mlinzi Ramos ilikua ni bahati mbaya.


Post a Comment