Rais
wa Heshima wa Timu ya Barcelona Kocha Johan Cruyff, akizungumza na
waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vilioko Zanzibar alipofika
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume.
Kikosi
cha Wachezaji wa Zamani wa Timu ya Barcelona wakiwa katika picha ya
pamoja baada ya kuwasili Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume
wakitokea Arusha , wakiwa Zanzibar kwa Mualiko wa Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, kutembelea
Zanzibar kujionea Vivutio vya Utalii na kujionea Vipaji vya wachezaji
Vijana wanaocheza katika timu mbalimbali za watoto.
Waandishi
wa habari za michezo Zanzibar wakiwa katika uwanja wa Ndege wa
Kimataifa kuipokea Timu ya Wachezaji wa Wazamani wa Timu ya Barcelona
Kikundi
cha ngoma wakitowa burudani wakati wa ujio wa Wachezaji wa zamani wa
timu ya Barcelona Zanzibar. kwa ziara ya siku moja Zanzibar. kwa mualiko
wa Rais wa Zanzibar Dk Shein.
Viongozi
wa Vyama vya Mpira Zanzibar wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wakiipokea timu ya Wachezaji wa zamani wa Barcelona walipowasili
Zanzibar.
Ndege
ya Serekali ikiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani
Karume ikiwa na Wachezaji wa Zamani wa Barcelona wakiwasili
Zanzibar kwa ziara ya siku moja kwa mualiko wa Rais wa Zanzibar Dk Ali
Mohemed Shein, na kujionea Vipaji vya Wachezaji wa timu za Watoto katika
uwanja wa Amaan Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Baraza la Taifa la Michezo Zanzibar Bi Shery Khamis akisalimiana na
mchezaji nyota wa timu ya wachezaji wa zamani wa Barcelona Kulvert
alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kwa ziara
ya siku moja Zanzibar.
Wachezaji
Nyota wa Timu ya Barcelona wakisalimiana na Viongozi wa Vyama vya
Michezo Zanzibar baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa
wa Abeid Amani Karume kwa ziara ya siku moja kwa mualiko wa Rais wa
Zanzibar Dk Shein.
Patrick Kluivert
No comments:
Post a Comment