Timu
ya Tanzania, FC Kilimanjaro ambayo ni mabingwa wa soka la Afrika nchini
Sweden imepata ushindi mnono wa mabao 6-1 dhidi ya watani wao wa jadi
Kenya kwenye mechi maalum ya kirafiki ya Amani na Upendo iliyofanyika
jijini Stockholm jana tarehe 11 Aprili, 2015
Mechi
hiyo iliandaliwa kwa pamoja na Balozi za Kenya na Tanzania nchini Sweden
kwa kushirikiana na wanadiaspora wa nchi hizo kwa madhumuni ya
kuonyesha mshikamano na kuziombea nchi zetu amani na upendo kufuatia
matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni nchini Kenya.
No comments:
Post a Comment