Pages

March 11, 2015

ZITTO KABWE ALIVYOVULIWA UBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI

Mnadhimu Mkuu Kambi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu, akitoa tamko la kumvua uanachama Zitto Zuberi Kabwe jana.
Waandishi wa habari wakifuatilia tukio hilo.
Lissu akitoa ufafanuzi baada ya kuulizwa maswali na wanahabari.
Katibu Mkuu wa Chadema Willbroad Slaa (kulia) akifuatilia mkutano huo wa kumvua uanachama Zitto Kabwe.MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Zuberi Zitto Kabwe, amevuliwa uanachama wake mchana huu katika ofisi za Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) jijini Dar es Salaam katika hatua iliyotangazwa na mnadhimu mkuu wa chama hicho, Tundu Lissu, baada ya mbunge huyo kushindwa kesi iliyokuwa amefungua katika Mahakama Kuu ya Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi hizo, Lissu alisema Zitto amefutwa uanachama kwa mujibu wa taratibu na sheria ya chama isemayo kwamba endapo mwanachama atapata tatizo lolote binafsi ama la kichama, malalamiko yote yatasuluhishwa ndani ya chama na si mahakamani.

“Hivyo, kwa mujibu wa sheria za chama, Zitto alikiuka sheria anapaswa kuvuliwa uanachama wake,” alisema Lissu.
Lissu aliongeza kuwa hata kama Zitto angeweza kwenda kushitaki lazima angeanzia katika mahakama ndogo za wilaya yaani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi au Masijala ya Mahakama ya Wilaya tofauti na alivyopeleka kesi hiyo moja kwa moja Mahakama Kuu.

Mahakama hiyo pia imemtaka mbunge huyo wa zamani kukilipa chama hicho gharama zote za kesi hiyo kama ilivyoelekezwa na mahakama, na kwa mujibu wa Lissu, Chadema kitakaa na kutathmini gharama husika.

Kuhusu utambulisho wa Zitto bungeni, Lissu alisema kwa mujibu wa kanuni za chama chake, katibu wa chama chake anatakiwa kumwandikia barua Mwenyekiti au Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi kumjulisha Zitto tena si mwanachama wao na taratibu zingine zitafuatia.

(PICHA/HABARI NA DENIS MTIMA/GPL)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...