Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akimpokea kwa furaha Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
alipowasili katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC ili kufanya
ufunguzi rasmi.
Mkurugenzi
wa Usimamizi wa Mikoa na Utawala wa NHC Bw. Raymond Mndolwa
akisalimiana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi alipowasili Longido kufungua rasmi nyumba za
ghrama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Williama Vangimembe Lukuvi
jana alifungua nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido na kuwataka wananchi kununua nyumba hizoili NHC iweze kujenga
zingine kusaidia Wilaya hiyo kupata makazi bora. Picha zote na Muungano
Saguya- Longido, ArushaMkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akikagua maandalizi ya ufunguzi
wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido, Arusha
kabla ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William
Vangimembe Lukuvi kufanya ufunguzi huo jana.
Hizi
ni nyumba za gharama nafuu zilizokamilika kujengwa na NHC Wilayani
Longido na ambazo ziko tayari kuuzwa kwa wananchi. Ufunguzi wa nyumba
hizi ulifanywa jana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Vangimembe Lukuvi
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na wafanyakazi wa
NHC waliokuwa wamejipanga kumpokea Waziri Lukuvi kufungua nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido.
Msafara wa Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
ukiingia eneo la mradi wa nyumba za gharama nafuu zilijengwa na NHC
Wilayani Longido ili kufungua rasmi nyumba hizo baada ya kukamilika
ujenzi wake.
Wafanyakazi
wa NHC nao hawakuwa nyuma kumpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi alipowasili mradi wa NHC
Longido kufanya ufunguzi rasmi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akifungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda,
Mbunge wa Longido Mhe. Lekule Laizer na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw.
Nehemia Mchechu.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa nyumba na kuingia ndani
kukagua nyumba hizo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akikagua vyumba mbalimbali vya nyumba bora zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido.
Wananchi
wa Wilaya ya Longido wakifuatilia kwa makini hotuba mbalimbali
zilizotolewa wakati wa ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa
na NHC Wilayani Longido
Mkurugenzi
Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Kyando Mchechu akitoa maelezo kwa Waziri wa
Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi ya
mradi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa Wilayani Longido.
Mkuu
wa Wilaya ya Longido Bw. Ernest Kahindi alitoa nasaha zake wakati wa
ufunguzi rasmi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani
Longido jana.
Watendaji
wa Wizara ya Ardhi Mkoani Arusha na wananchi wakifuatilia matukio ya
ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC Wilayani Longido
jana.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda akilishukuru Shirika la Nyumba
kwa kujengwa nyumba Wilayani Longido eneo ambalo ni kame na lenye
changamoto kubwa ya kutekeleza ujenzi wa nyumba bora
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akihutubia halaiki ya wananchi wa Longido (hawapo pichani)waliohudhuria
ufunguzi alioufanya wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC
Wilayani humo.
Mbunge
wa Longido Mhe. Lekule Laizer akilishukuru Shirika la Nyumba kwa
kuiweka Wilaya ya Longido katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa
ujenzi wa nyumba za gharama nafuu zinazojengwa na NHC katika Halmashauri
mbalimbali za Wilaya hapa nchini.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akikagua nyumba za makazi zilizojengwa na NHC eneo la Levolosi Jijini
Arusha.Nyumba hizi zinauzwa kwa wananchi.
No comments:
Post a Comment