Pages

March 21, 2015

WAZIRI WA ARDHI,NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI AENDELEA KUSIKILIZA KERO ZA ARDHI MKOA WA MANYARA

Katibu Tawala  wa mkoa wa Manyara,Mhandisi Omar  Chambo akisoma taarifa ya migogoro ya ardhi mkoani humo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Vangimembe Lukuvi kwenye ziara yake ya kusikiliza kero za ardhi.

Mkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika  kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza  katika  kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara  kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.

Mratibu wa Tume ya Waziri Mkuu ya kuhakiki na kuweka mipaka kwenye maeneo yenye migogoro ya ardhi mkoani Manyara,ambaye pia ni Mrasimu Ramani Mwandamizi,Bw.Benedict Mugambi akitoa maelezo ya hatua waliyofikia katika kuweka mipaka mkoani Manyara na kusema kuwa migogoro mingi ya mipaka inasababishwa na wanasiasa.

Baadhi ya watendaji wa sekta ya Ardhi Kanda ya Kaskazini na baadhi ya waheshimiwa wabunge akiwemo Mbunge wa Kiteto,Benedct Ole Nangoro na Mbunge wa Viti Maalum,Pauline Gekul wakifatilia maelekezo ya Mhe Lukuvi alipozungumza na watendaji wa mkoa wa Manyara 

Wananchi wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi(hayupo pichani)alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.

Wananchi wa mkoa wa Manyara wakipeana maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza  na wananchi wa mji wa Babati waliojitokeza kuwasilisha kero zao zinahusu  migogoro ya ardhi.Kikao hicho kilihudhuriwa pia na wabunge wa mkoa wa Manyara.

Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akipokea barua zilizowasilishwa na wananchi mbalimbali waliodai kudhurumiwa haki zao na watendaji wa idara ya ardhi.

Baadhi ya watendaji wa wizara ya ardhi wakiratibu malalamiko ya wananchi katika kikao kilichofanyika ofisi za halmashauri ya wilaya ya Babati,mkoa wa Manyara.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...