Sehemu ya nyumba 40 za gharama
nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati mkoani Manyara ambazo
zilifumguliwa rasmi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
……………………………….
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi amehitimisha ziara
yake ya kutatua migogoro ya Ardhi katika mikoa ya Mwanza, Arusha na
Manyara na ameweza pia kuweka jiwe la msingi mradi wa nyumba za gharama
nafuu Buswelu Mwanza na kufungua nyumba za aina hiyo zilizojengwa na NHC
katika eneo la Longido Arusha na Mrara Babati. Picha za ufunguzi wa
Mradi wa Mrara na Muungano Saguya-Babati
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia
Kyando Mchechu akitoa maelekezo kwa watendaji wake muda mfupi kabla ya
ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara
Babati mkoani Manyara
Kikundi cha sanaa kikiburudisha
halaiki ya wananchi( haiku pichani) iliyohudhuria ufunguzi uliofanywa na
Waziri Lukuvi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la
Mrara Babati mkoani Manyara.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia
Kyando Mchechu akionyeshwa mipaka ya eneo linalomilikiwa na NHC na
Msimamizi wa Mradi wa NHC Mrara Babati Bi Linda Kasilima baada
Mkurugenzi Mkuu kubaini kuwepo kwa uvamizi wa baadhi ya viwanja vya
Shirika. Kufuatia hali hiyo Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Bendera
ameagiza wote waliovamia viwanja hivyo kunyang’anywa mara moja na nyumba
zao kuvunjwa bila fidia.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia
Kyando Mchechu akimpokea Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. William Vangimembe Lukuvi alipowasili katika mradi wa nyumba za
gharama nafuu unaotekelezwa na NHC ambapo aliifungua rasmi baada ya
kukamilika. Nyjmba hizo 40 sasa zinauzwa kwa wananchi mbalimbali wa
Babati na nje ya Wilaya hiyo wanaohitaji.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akivishwa skafu na
skauti kuashiria alama ya amani, upendo na mshikamano mara alipowasili
kufungua rasmi nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la rara
Babati.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitambulishwa na
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia Mchechu Msimamizi wa mradi wa nyumba
za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati Bi. Linda
Kasilima alipowasili kufungua rasmi nyumba hizo.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akifunua kitambaa
kuashiria ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo
la Mrara Babati. Nyumba hizo zimeshakamilika na zinauzwa kwa wananchi
wanaohitaji wa Bbati na nje ya Babati.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akikata utepe kufungua
nyumba iliyotayarishwa kuwakilisha ufunguzi rasmi wa nyumba 40 za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati. Kulia kwake ni
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel Nkaya Bendera, Mbunge wa Babati
Vijijini Mhe. Jituson Vrajilal na Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia
Mchechu .
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akitoka katika nyumba
ya mfano aliyoifungua baada kukagua vyumba na ubora wa nyumba
zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Mkurugenzi Mkuu wa NHC Bw. Nehemia
Kyando Mchechu akitoa maelezo ya mradi kwa Mhe. Waziri wa Ardhi na
halaiki ya wananchi wa Babati(hawapo pichani) waliohudhuria sherehe za
ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara
Babati.
Sehemu ya halaiki ya wananchi
waliohudhuria ufunguzi wa nyumba zilizojengwa na NHC eneo la Mrara
Babati uliofanywa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi.
Mkuu wa Wilaya ya Babati Bw.
Crispin Meela akisalimia wananchi na kumkaribisha Mkuu wa Mkoa wa
Manayara kusalimia wananchi katika sherehe za ufunguzi wa nyumba za
gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Joel
Bendera akihutubia wananchi na kusisitiza maafisa ardhi na mipango miji
kufuata sheria katika usimamaizi na utoaji haki za ardhi Mkoani humo
wakati wa sherehe za ufunguzi wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na
NHC eneo la Mrara Babati.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na
Maendeleo ya Makazi Mh. William Vangimembe Lukuvi akihutubia wananchi na
kusisitiza Halmashauri za Wilaya kutenga ardhi kwa ajili ya kuwezesha
NHC kujenga nyumba nafuu alipofungua rasmi nyumba za gharama nafuu
zilizojengwa na NHC eneo la Mrara Babati.
Mbunge wa Babati Vijini Mhe. Mhe.
Jituson Vrajilal akitoa neon la shukrani kwa NHC kwa kuwezesha Wilaya ya
Babati kupata nyumba bora na kusaidia vijana mashine za kufyatulia
matofali huku akichagiza VETA na taasisi zingine zihusike kusaidia
vijana.
Mbunge wa Viti maalum Paulina
Gekul akisalimia wananchi na kumpongeza Waziri Lukuvi kwa kuacha ofisi
ili kusikiliza kero za wananchi hali aliyosema inafaa kuigwa na Mawaziri
wengine.
No comments:
Post a Comment