Watu
watatu wanaume wasiofahamika, wamekutwa wamekufa na kutelekezwa maeneo
ya Mjohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, huku miili yao ikionesha
majeraha maeneo tofauti pamoja na kuvuja damu nyingi puani.
Kamanda
wa polisi mkoani Kilimanjaro, Geofrey Kamwela (pichani) alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo, lakini akasema ametuma maofisa wake eneo la
tukio na taarifa rasmi ataitoa itakapokamilika.
Taarifa
za awali zinaeleza kuwa marehemu hao wanakadiriwa kuwa na umri wa kati
ya miaka 28 na 32 wanadhaniwa ni wachimbaji wa madini ya Tanzanite wa
Mirerani mkoani Arusha.
Kwa
mujibu wa taarifa kutoka kwa wakazi wa maeneo ilipokutwa miili hiyo
ambao walizungumza kwa sharti la kutotajwa majina yao miili hiyo
ilikutwa eneo jirani na alipouawa bilionea wa madini ya Tanzanite mkoani
Arusha, marehemu Erasto Msuya aliyeuawa kupigwa risasi kifuani.
Mmoja wa
mashuhuda wa tukio hilo alisema askari kutoka kituo cha Bomang'ombe
walifika eneo la tukio majira ya saa 3:00 za asubuhi na kufanya
uchunguzi katika eneo la tukio na kisha wakaondoka na miili ya vijana
hao.
No comments:
Post a Comment