Pages

March 2, 2015

WAFANYE WATABASAMU WATABASAMU NA WATOTO MUHIMBILI

 Mratibu wa programu ya Wafanye Watabasamu na mchora vibonzo maarufu nchini, Nathan Mpangala, akimwonesha mtoto Maurine jinsi ya kuchora katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita. Mpangala na wenzake walitembelea watoto wanaotibiwa saratani ili kuchora nao na kuwapa zawadi mbalimbali. Zaidi kuhusu programu hii tembelea: https://www.facebook.com/wafanyewatabasamu
 Nguvu ya sanaa tiba kama inavyooneshwa na Clara.
 Sanaa tiba ikawasahaulisha maumivu, wakajihisi wako nyumbani. Baadhi ya watoto wakijiachia na marafiki wa Wafanye Watabasamu waliokwenda kuwatabasamisha katika hospitali ya Taifa Muhimbili, Jumamosi iliyopita.
 Mtoto Nico akienda sambamba na marafiki wa Wafanye Watabasamu. Kutoka kulia ni Sia Marupa, Masoud Junior na Cloud Chatanda.
 Sanaa tiba ikapandisha mzuka, viganja vikazungumza kama inavyoonekana kwa mtoto Heri. Wafanye Watabasamu inakuombea upate nafuu ya mapema.
 Ha ha ha haaaaaa. Hili ndilo lengo hasa la Wafanye Watabasamu. Mungu akupe nafuu ya mapema Nico.
 “Tukikosea je?!” Swali alilouliza mtoto Clara na kuzua kicheko. Aliliuliza baada ya mchoraji Paul Ndunguru aliyeipa kamera mgongo kusema kuwa wachore huku wamefumba macho. Kutoka kushoto: Tatu Bendera, Mama Pili Mtambalike na Beatrice Makelele.
 Baadhi ya watoto na marafiki wa Wafanye Watabasamu wakionesha kazi zao.
 Kulikuwa na aina mbalimbali za sanaa tiba. Komediani Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga (kulia) alikuwa kivutio kwa watoto.
 Mtoto Clara (kulia) akiwa na rafiki wa Wafanye Watabasamu, Arafa Salim.
 Rafiki wa Wafanye Watabasamu ambaye pia ni gwiji la uchoraji nchini, Paul Ndunguru, akiangalia umahiri wa uchoraji wa mtoto Clara wakati wa zoezi la sanaa tiba.
Hakika sanaa tiba ni dawa. Mtoto Henry alidhihirisha kuwa hata naye komedi iko damuni. Toka kulia; Abdul Kingo, Faiza Ally, Fred Halla, Wakuvwanga, Amani Abeid na Lute Mwakisopile. (Picha zote na Wafanye Watabasamu).
Links:

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...