Makau wa Rais Kenya, William Ruto ndani ya Mahakama ya ICC.
Serikali
ya Kenya imeutambua rasmi mwili wa mtu mmoja uliopatikana katika mbuga
ya wanyama ya Tsavo, kuwa ni wa Meshack Yebei ambaye alikuwa shahidi
katika kesi inayomkabili makamu wa rais wa Kenya William Ruto. kwenye
Mahakama ya ICC.Mkemia
wa serikali ya Kenya ametangaza kuwa mwili huo ambao ulikuwa
umehifadhiwa kwenye chumba cha maiti tangu mwezi December mwaka 2014 ni
wa Meshack baada ya mwili huo kufanyiwa uchunguzi wa chembechembe za
DNA.
Meshack Yebei
Meshack
Yebei alitekwa mwishoni mwa mwezi December nyumbani kwake Eldoret
alipokwenda kumwona mkewe aliyekuwa anaumwa, familia yake ililalamika
kuwa kutoweka kwa Yebei kunatokana na kuhusishwa na kesi hiyo.
Yebei
alitarajiwa kuwa shahidi wa Makamu wa Rais wa Kenya, William Ruto kwenye
kesi yake ya mauaji inayoendelea Mahakama ya ICC, The Hague.
Marehemu
alipewa nafasi ya kupata ulinzi na makazi salama lakini akakataa,
Serikali ya Kenya itafanya uchunguzi kugundua kilichosababisha kifo
chake.
No comments:
Post a Comment