Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh.
Mahmoud Thabit Kombo akipitia kijarida cha maelezo kazi zinazofanywa na
taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15. Kushoto ni Mwenyekiti wa
taasisi hiyo, Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi
hiyo uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye hoteli ya Hyatt Regency jijini
Dar.(Picha na Zainul Mzige wa modewjiblog).
Na Mwandishi wetu
NAIBU
Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi, Mahmoud Thabit Kombo ameitaka
jamii kubadili utamaduni na kumshikirisha mwanamme wakati mke wake
akienda kujifungua ikiwa ni sehemu ya kuhakikisha usalama wa mtoto na
mama.
Alisema
wanaume wengi hasa wanawake wao wanapokuwa wajawazito na wanakaribia
kujifungua wanakosa amani na wengine hukimbia nyumbani au humkimbiza mke
na mtoto wao kwa ndugu na jamaa baada ya kujifungua kutokana na kukosa
ushauri unaompa ujasiri kuhusu familia yake hiyo mpya.
Naibu
waziri huyo alitoa kauli hiyo wakati wa uzinduzi wa taasisi
inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel mwishoni mwa
wiki.
Alisema
yeye anaamini kwamba moja ya vitu vinavyoweza kupunguza idadi ya vifo
kwa watoto wa njiti ni ushiriki wa wanaume na kuwataka watu wa Doris
Mollel Foundation kufanya kampeni kubwa ya kubadili tamaduni na wanaume
kukalishwa chini kuelekezwa.
Muuguzi
wa wodi ya watoto katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mariana Makanda
akitoa somo na elimu ya makuzi kwa watoto njiti wanaozaliwa nchini
kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
Aidha
ushiriki wa wanaume katika ujauzito umeelezwa kusaidia kuondoa
mashinikizo na ukosefu wa lishe bora kwa wawanake wajawazito kutokana na
vitu hivyo kuwa sehemu ya uzazi wa watoto njiti.
Alisema
pamoja na kutoa elimu kwa wanaume na wanawake hasa wauguzi juu ya haja
ya wanaume kuona mahangaiko ya wanawake zao, ameitaka jamii kutambua
kwamba uzazi katika umri mdogo ni tatizo jingine linalopsababisha uzazi
wa watoto njiti.
Alisema
kuhusu mabadiliko katika hospitali na zahanati zetu ili kuwa bora kwa
uzazi salama Naibu waziri huyo alitaka taasisi mbalimbali kushirikiana
na serikali kuhakikisha kwamba si watoto njiti tu wanakuwa salama bali
hospitali na zahanati hizo zinakuwa salama kwa uzazi wa aina zote.
Awali
wakati akimkaribisha Naibu Waziri kufungua taasisi hiyo, Balozi
Mwanaidi Sinare, alisema kwamba ipo haja ya zahanati na hospitali za
Tanzania zikawa katika hali ya kupokea uzazi wa aina zote ili watoto
njiti waweze kuendelea kuishi.
Mgeni
rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh.
Mahmoud Thabit Kombo akizungumza kwenye uzinduzi wa taasisi ya Doris
Mollel uliofanyika mwishoni mwa juma kwenye hotel ya Hyatt Regency
jijini Dar.
Wakati
huo huo mwasisi wa taasisi hiyo ambaye pia ndiye Mwenyekiti wake, Doris
Mollel ambaye ni Mrembo wa Singida 2014/15, ambaye alisema kwamba yeye
alizaliwa akiwa njiti na uzito wa kilio 1.2 alisema zaidi ya watoto
200,000 huzaliwa njiti kila mwaka huku elfu 9 wakifariki.
Alisema
wengi wa watoto hao hufariki kwa kukosa huduma muhimu hasa mashine za
kuwawezesha kunyonya, kupata joto kuendelea kuishi kabla ya kutoka
hospitalini.
Alisema lengo la kuanzisha taasisi hiyo ni kutafuta fedha za kuweza kusaidia watoto njiti ili kupunguza vifo na kuviondoa.
Watoto njiti milioni 15 huzaliwa duniani na kati yao milioni 1 hufa wengi wao kutoka nchi zinazoendelea ikiwamo Tanzania.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akielezea
makuzi yake baada ya kuzaliwa njiti wa uzito wa kilio 1.2 na kuona
kuna umuhimu wa kusaidia watoto njiti wasipoteze maisha kutokana na
kukosa vifaa vya kufanya watoto hao waweze kuishi na kufikia malengo
kama watoto wengine ambao hawakuzaliwa na wakiwa njiti.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel
akimpongeza Balozi Mwanaidi Sinare kwa risala nzuri aliyoitoa wakati wa
sherehe za uzinduzi wa taasisi hiyo uliofanyika katika hoteli ya Hyatt
Regency mwishoni mwa wiki jijini Dar. Kulia ni mgeni rasmi Naibu Waziri
wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo akizungumza na kumpongeza
Doris Mollel wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa taasisi hiyo.
Meza kuu wakijianda kuelekea sehemu maalum ya kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa taasisi hiyo.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel na
mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba kwa pamoja wakikata utepe
kuzindua taasisi yao huku Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo (kushoto) na Balozi Mwanaidi Sinare
wakishuhudia tukio hilo.
Sasa imezinduliwa rasmi.
Balozi
Mwanaidi Sinare (kulia) akimpongeza Mwenyekiti wa taasisi
inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel ambaye pia
ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel kwenye uzinduzi huo.
Sehemu
ya ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria uzinduzi wa taasisi ya Doris
Mollel uliofanyika mwishoni mwa wiki kwenye Hoteli ya Hyatt Regency
jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau waliohudhuria uzinduzi huo.
Meza kuu kwa pamoja wakikata cake maalum wakati wa uzinduzi huo.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha
cake mgeni rasmi Naibu Waziri wa Afya wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, Mh. Mahmoud Thabit Kombo wakati wa uzinduzi.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha
cake Balozi Mwanaidi Sinare.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel
akimlisha cake Muuguzi wa wodi ya watoto Hospitali ya Taifa Muhimbili,
Mariana Makanda (kushoto).
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha
kipande cha cake mshirika mwenza wa taasisi hiyo Heena Mujtaba.
Mwenyekiti
wa taasisi inayoshughulikia na utetezi wa watoto njiti ya Doris Mollel
ambaye pia ni Miss Singida Kanda ya Kati 2014/15, Doris Mollel akimlisha
kipande cha cake mama yake mzazi Celina Mollel.
Rachel Temu, William Malecela pamoja na mdau wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel.
Kaimu
Mkurugenzi wa Idara ya Diaspora kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bibi Rosemary Jairo (kulia) Mdau wa Doris
Mollel Foundation, Suleiman Saleh pamoja mgeni mwalikwa.
Aliyekuwa
Miss Tanzania 1999, ambaye pia ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano
wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu (kushoto) akifurahia jambo
wakati wa uzinduzi wa taasisi ya Doris Mollel. Kulia ni Miss Tanzania
1998, Basila Mwanukuzi (kulia).
Mtangazaji wa kituo cha Channel Ten na Magic FM, Salma Msangi na rafiki yake wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi
ya wageni waalikwa akiwemo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Jambo
Concepts ambao ni Wachapishaji wa Magazeti ya Jambo Leo, Juma Pinto (wa
tatu kulia) na Mkurugenzi wa Kampuni ya Jambo Concepts, Benny Kisaka (wa
pili kulia) wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment