Soko la Mchikichini, Ilala-Boma linavyoonekana kufuatia mvua za sasaMaji yalivyotapakaa soka la Sinza Afrika-Sana.
WAKATI
mvua zikiendela kunyesha katika jiji la Dar es Salaam, na sehemu
nyingine nchini, wakazi wake wengi wameonekana kuhangaika kupata sehemu
salama za kuishi na kufanyia biashara.Mtandao huu umezungukia maeneo
mbalimbali ya jiji na kukuta wakazi wa maeneo mengi wakitoa maji kwenye
nyumba zao na sehemu za kufanyia biashara.
Wakiongea
na mwandishi wetu, wakazi wa maeneo ya Mwanayamala-Mkwajuni maarufu
kama Bondeni, wameitupia lawama kampuni ya ujenzi ya Strabag kuwa
imechangia nyumba zao kuingiliwa na maji kwani mifereji iliyotengenezwa
haikidhi uwezo wa kusafirisha maji kwa kasi kwani ni midogo na badala
yake maji hujaa na kuelekea katika makazi yao.
Katika
maeneo ya Jangwani mtandao huu ulikuta baadhi ya nyumba zilizoko bondeni
zikiwa karibu kumezwa na maji, ambapo wakazi wa maeneo hayo wametaka
serikali iwasaidie.
Katika
soko la Sinza Afrika-Sana, wafanyabiashara ndogondogo wa soko hilo
wameelezea kero inayosababishwa na mifereji inayopitisha maji barabarani
kuziba kufuatia uchafu unaotupwa ovyo na hivyo kuelekeza maji katika
biashara zao na wateja kukosa sehemu ya kupita.
Vilevile,
wafanyabiashara ndongondogo eneo la Ilala-Boma katika soko la
Mchikichikini, wamesema mvua zinazoendelea zinawafanya wengi wao kukosa
fedha ya kujikimu kutokana na wateja kutokufika kwenye vibanda vyao
kwani maji yanajaa sehemu hizo zaq biashara.
(STORI/PICHA NA DENIS MTIMA/GPL)
No comments:
Post a Comment