Maafisa polisi wawili wapigwa risasi katika jimbo la Ferguson, katika mji wa Missouri uliokumbwa na machafuko yanayohusiana na kuuwawa na polisi kijana mdogo mweusi asiye na silaha mwaka jana.
Mkuu wa Polisi wa Kituo cha Kaunti ya St. Louis Jon Belmar amesema afisa polisi mmoja amepigwa risasi usoni na mwingine kwenye bega na kujeruhiwa vibaya, hata hivyo hawajapoteza fahamu.
Polisi hao wa Marekani wamepigwa risasi wakati wa maandamano yaliyofuatia kujiuzulu kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi wa Ferguson, kufuatia ripoti iliyoibua suala la ubaguzi wa rangi katika idara ya polisi.
Waandamanaji uso kwa uso na polisi
Polisi wakimdhibiti muandamanaji
No comments:
Post a Comment