Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akiingia jengo la Utawala la Mkoa wa Arusha ili kukutana na Uongozi wa
Mkoa huo kupata taarifa ya Mkoa inayohusu migogoro ya ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akipokelewa na Uongozi wa Mkoa wa Arusha alipowasili kufanya ziara ya
kusikiliza na kutatua kero za ardhi zilizoko katika Halmashauri
mbalimbali za Mkoa huo.
Baadhi
ya watendaji na viongozi mbalimbali wa Halamashauri za Mkoa wa Arusha
wakimsikiliza Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Lukuvi alipowakutanisha katika Hoteli ya Naura Springs
kuzungumzia kero na migogoro ya ardhi katika mkoa huo kwa nia ya
kuipatia ufumbuzi wa haraka.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akielezea mambo mbalimbali yahusuyo ardhi na mipangomiji kwawatendaji wa
Mkoa wa Arusha(hawapo pichani) alipozungumza nao kwenye hoteli ya Naura
Springs Arusha jana. Waziri Lukuvi amesisitiza nidhamu ya kazi na
kufuata sheria katika kuhudumia wananchi masuala yahusuyo ardhi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akikabidhiwa makabrasha yenye kero mbalimbali za ardhi zilizowasilishwa
kwake kwa ufasaha mkubwa na Mkoa wa Arusha kupitia Mpima Ardhi wa Mkoa
wa Arusha Bw. Hamdoun Mansoor.
Mbunge
wa Arumeru Magharibi Mhe. Goodluck Ole Medeye naye alikuwepo hoteli ya
Naura Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye
mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Vangimembe Lukuvi
Mbunge
wa Arusha Mhe. Godbless Lema naye alikuwepo hoteli ya Naura Spring
kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye mkutano
ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.
William Vangimembe Lukuvi.
Mbunge
wa Arumeru Mashariki Mhe. Joshua Nassari naye alikuwepo hoteli ya Naura
Spring kuzungumzia migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi kwenye
mkutano ulioandaliwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mhe. William Vangimembe Lukuvi.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Felix Ntibenda akiwakemea watendaji wa ardhi Mkoani
Arusha kutokana na umangimeza wao unaowafanya kushindwa kutatua kero za
ardhi na kusababisha migogoro mingi ya ardhi mkoani humo. Alisema
maafisa ardhi na mipango miji wanalalamikiwa sana na wananchi.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akiongea na waandishi wa habari katika eneo lenye mgogoro wa ardhi
lililoko mpaka wa Longido, Monduli na Arumeru eneo la Oldonyosambu
Arusha. Waziri ameahidi kukutana na wanasiasa wa Mkoa wa Arusha ili
kumaliza mgogoro huo.
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Vangimembe Lukuvi
akionyeshwa na Mpima Ardhi wa Mkoa wa Arusha Bw. Hamdoun Mansoor ramani
yenye mipaka katika maeneo yanayobishaniwa kwenye mgogoro wa ardhi kati
ya Wilaya za Arumeru, Monduli na Longido.
Arusha.
Waziri
wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,William Lukuvi ameipa mwezi mmoja halmashauri ya wilaya ya Meru mkoa wa Arusha kufanya
tathmini ya mashamba 11 yenye ukubwa wa zaidi ya hekari 7,000 ambayo Rais
alifuta hati milki zake ili yatolewe kwa wananchi.
Kauli hiyo
imetolewa jana kwenye kikao cha viongozi wa halmashauri tatu za Jiji la Arusha,Arusha
DC na Meru katika ziara ya siku ya kutatua migogoro ya ardhi ambayo imekua kero
kwa muda mrefu.
“Kuna
mashamba 11 ambayo Rais amefuta umiliki wake wa awali kutokana na kukiuka sheria,nataka
mfanye tathmini ya mali na maendelezo na sio ardhi,ardhi ni mali ya Rais ambayo
ameishaichukua,hivyo mtakapofanya tahmini mzingatie hilo,”alisema Lukuvi
Alisema
katika kuwaondolea kero wananchi kupata ardhi kwa gharama nafuu watakaopata
mashamba hayo ataondoa kodi kuu ambayo ana mamlaka nayo lengo likiwa
kuwawezesha kupata ardhi ambayo wengi wao wamekua wakiishi kama manamba.
Mbunge wa
Arumeru Magharibi,Godluck Ole Medeye alisema migogoro ya ardhi imekua ya muda
mrefu ambayo imekua kero na kusababisha
uvunjifu wa amani jambo ambalo halina tija kwa nchi.
Alisema
migogoro ya mipaka wilaya ya Arumeru ,Monduli na Longido ni mfano mbaya ambao
wananchi wanaoishi kwenye maeneo hayo unawakosesha utulivu wa kujiendeleza.
Kwa upnde
wake Mbunge wa Arusha Mjini,Godbless Lema alisema wizara ya Ardhi na Wizara ya
Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa likae pamoja kuona umuhimu wa kuhamisha kambi
ya Jeshi ya Tanganyika Packers kuhamishwa kwani sio busara kuwa katikati ya
makazi kutokana na jiji la Arusha kukua kuelekea Kusini ambao wapo kwenye
shamba la Themi holding Group.
Katika hatua
nyingine Lukuvi alisema serikali imetanga kiasi cha Sh 8 bilioni kutengeneza
ramani ya mipango miji kwenye majiji ya Mwanza na Arusha ili iendane na miji
mingine kimataifa.
Awali Afisa Ardhi wa Mkoa wa Arusha,Hamdun Mansoor
alitaja baadhi ya migogoroinayotishia amani kuwa ni pamoja mgogoro wa mpaka
mikoa ya Arusha na Simiyu kwenye Kijiji cha Kakesio wilaya za Ngorongoro na
Meatu,Shamba la Valesca lililopo wilaya ya Arumeru na shamba la Ndarakwai
ambalo liko wilaya ya Longido na Hai mkoa wa Kilimanjaro.
Migogoro
mingine ni tamko la kuanzishwa hifadhi za taifa bila kuchora ramani jambo
linaloingiza baadhi ya vijiji ndani ya hifadhi hizo na kusababisha migogoro.
No comments:
Post a Comment