UFUATAO
ni ujumbe mfupi wa Muadhama Polycarp Kardinali Pengo alioutoa leo katika
Kanisa la St. Joseph jijini Dar es Salaam kuhusiana na waraka wa
maaskofu uliotolewa hivi karibuni kwa Wakristo nchini kujiandikisha
kikamilifu na kisha kuikataa Katiba Inayopendekezwa wakati wa kura ya
maoni kwa vile haikujadiliwa kiuadilifu.
"Maaskofu
hatuna mamlaka ya kuwaamulia/kuwalazimisha waumini wetu wafanye uamuzi
gani kuhusu katiba, kuwaamulia ni kuwadharau kuwa hawawezi kufanya
uamuzi sahihi wao wenyewe na kuingilia uhuru wao.
Waraka huu unaleta utengano katika taifa kuwa Wakristo, tumechukua uamuzi dhidi ya serikali na wengine....
Tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa tafakari yao binafsi bila shinikizo letu.....
Wakati
hili linajadiliwa nilikuwa Italy katika kusimikwa makardinali na baadaye
India, wengine wakavumisha nimelazwa,..wengine nimefariki, lakini
namshukuru Mungu hizo ni dua za kuniongezea maisha marefu na afya
(makofi).
Nililetewa
waraka nikausoma, umepitishwa baada ya tafakari kubwa nauheshimu.
Lakini nadhani tuwaache waumini wafanye uamuzi kwa uhuru baada ya
kutafakari....
Si sahihi tukaenda katika katiba kama Wakristo kwa shinikizo la kupinga katiba...
Wawe huru anayepinga kwa hiari yake anayekubali kwa dhamiri yake....
Sidhani kama viongozi wa dini sasa tuna amri ya kulazimisha uamuzi juu ya katiba....
No comments:
Post a Comment