Naibu Waziri Sayansi na
Teknolojia January Makamba akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya na
kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
Afisa Mtendaji Mkuu wa
CMEA, Paul Matthysse akisisitiza jambo wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo yenye
lengo la kuwakwamua wanamuziki katika umaskini. CMEA pia itawawezeha pia
watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari kupata
kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na kwa
mwaka.
Mwanamuziki Mkongwe nchini,
John Kitime akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na
Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kwa
jina la Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
Meneja Mradi wa kampuni ya
Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) ambayo inasimamia haki miliki
za kazi za wasanii wa ukanda wa nchi ya Afrika Mashariki, Abdi Zagar akielezea
jinsi kampuni yao inavyofanya kazi wakati wa uzinduzi wa kampuni hiyo.
Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, January Makamba akisalimiana na Afisa Mteandji Mkuu wa Chama Cha
Hakimiliki Tanzania, Doreen Sinare wakati w uzinduzi wa kampuni ya
inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika
Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East Africa Limited
(CMEA). Katikati ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (Basata),
Godfrey Mngereza.
Afisa Mteandji Mkuu wa
Chama Cha Hakimiliki Tanzania, Doreen Sinare wakati w uzinduzi wa kampuni ya
inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika
Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East Africa Limited
(CMEA).
Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, January Makamba akiwa katika “red carpet’ wakati wa uzinduzi wa
kampuni ya inayojishughulisha na Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za
Afrika Mashariki ijulikanayo kwa jina la Copyrights Management East Africa
Limited (CMEA).
Banana Zorro wa B-Band
akiwa na Mwenzake wakati wa uzinduzi wa kampuni ya inayojishughulisha na
Hakimiliki za kazi za wasanii katika nchi za Afrika Mashariki ijulikanayo kwa
jina la Copyrights Management East Africa Limited (CMEA).
Na Mwandishi
Wetu
Naibu Waziri wa Sayansi na
Teknolojia, January Makamba amewataka wanamuziki nchini kuachana na kutegemea
kupata shoo za majukwaani na kupata umaarufu usiokuwa na tija kwa kujiunga na
kampuni ya Copyrights Management East Africa Limited (CMEA) ambayo inasimamia
haki miliki za kazi za wasanii wa ukanda wa nchi ya Afrika
Mashariki.
Naibu Waziri Makamba
alisema hayo wakati wa uzinduzi rasmi wa kampuni ya CMEA ambayo ipo chini ya
mtayarishaji wa muziki maarufu, Paul Matthysse (P-Funk) ambaye ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa kamuni hiyo.
Makamba alisema kuwa
wanamuziki wengi nchini wanapata umaarufu mkubwa wa bila kipato kutokana na kazi
zao bora kwani hawafaidiki na utunzi wa nyimbo zao zinazopigwa kwenye
televisheni na vituo vya redio mbalimbali.
Alisema kuwa matokeo yake
wanapotea katika fani hiyo na kuwa maskini maarufu na faida kubwa kwao ni kupata
sifa kwa warembo mbalimbali ambao huwakimbia pale wanaposhuka katika
fani.
“Mimi najua muziki na
wanamuziki, hakuna mtu anayeweza kunidanganya, wanamuziki wanapata tabu katika
utunzi na baadaye kutafuta fedha za kurekodi kwa kukopa au kwa kuombaomba,
baadaye watafute fedha za kuwapa madj wa redio na wa vipindi vya televisheni ili
wimbo wake uchezwe na kupata shoo mbalimali kwa kipato kidogo,” alisema
Makamba.
Alisema kutokana na hali
ilivyo, mwanamuziki anaishia kukuapata shoo kwa ujira mdogo na akipotea katika
fani, anakuwa maskini maarufu.
“CMEA ni sululisho kwenu,
kampuni hi itafanyakazi pamoja na Chama Cha Hakimiliki Tanzania (Cosota) kuweza
kujua wimbo wako au video yako imechezwa mara ngapi redioni au kwenye
televisheni na unastahili kulipwa shilingi ngapi,” alisema. Alisema kuwa hata
baada ya kuacha muziki, utaendelea kupata fedha ‘pensheni’ kutokana na wimbo au
video yako kuchezwa redioni na kwenye televisheni.
Afisa Mtendaji Mkuu wa
CMEA, Paul Matthysse alisema kuwa mbali ya wanamuziki, kampuni yao itawawezeha
pia watayarishaji wa muziki na wasanii wengine pamoja na vyombo vya habari
kupata kufahami takwimu sahihi za nymbo zilizochezwa kwa siku, wiki, mwezi na
kwa mwaka.
Matthysse alisema kuwa
kampuni yao imewekeza mitambo ya kisasa inayowezesha kuchapisha na kuhakiki
nyimbo pindi zinapochezwa hewani na televisheni na redio na kutoa ripoti za aina
mbalimbali zinazohitajika kutumika kwa malengo maalum.
“Pia tunapokea na kuhifadhi
nyimbo kwenye mitambo maalum kwa matumizi ya uhakiki, na kudhibiti kiasi cha
mirabaha ambacho Cosota kupitia vyombo vya habari inatakiwa kuwalipa wasanii
kulingana na idadi kamili ya urushwaji wa kazi zao,” alisema Matthys
No comments:
Post a Comment