Pages

March 6, 2015

AJUZA ASHEHEREKEA SIKU YAKE YA KUZALIWA BAADA YA KUTIMIZA MIAKA 117

 Ajuza raia wa japan Misao Okawa (117) akiwa na familia yake. Ajuza huyu bado yupo katika afya njema na hata msosi anaupiga kama kawaida.
Ajuza raia wa japan Misao Okawa (117) leo amefanya Birthday yake ya kuzaliwa akiwa 117 akiwa ndiye mtu aliyekula chumvi nyingi duniani.

Okawa aliyezaliwa Machi 5, 1898 ameifurahia siku yake hiyo akiwa na familia yake.

Akizungumza Misao Okawa amesema kuishi miaka 117 sio kitu alicho kizania. 

Ajuza huyo sasa analelewa katika kituo maalum cha wazee kilichopo katika mji wa Osaka na wahudumu katika kituo hicho wanasema kuwa, Okawa katika miezi ya karibuni amepunguza uwezo wake wa kusikia.

Ajuza huyo alifunga ndoa  mwaka 1919 na Yukio ambaye alifariki mwaka 1931 wakiwa wamezaa watoto watatu kati yao wasichana wawili na mvulana mmoja ambapo sasa anawajukuu wanne na vitukuu 6. 

Alitambuliwa rasmi kuwa ndiye mtu mzee kuliko wote duniani mwaka 2013 na kitabu cha kumbukumbu Duniani cha Guinness.Source: BBC-UK

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...