Pages

February 3, 2015

Waziri wa Ujenzi aanza ziara ya Ukaguzi wa barabara mikoani ya Rukwa na Katavi

Mamia ya wakazi wa Tunduma wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli mara baada ya kumsimamisha alipokuwa njiani kuelekea mkoani Rukwa kwa ajili ya Ukaguzi wa barabara za mkoa huo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi hao wa Tunduma.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiagana na wananchi wa Tunduma mara baada ya kuwahutubia na kuwaahidi ujenzi wa barabara ya Tunduma mjini kwa njia nne ili kupunguza kero ya msongamano wa malori katika eneo hilo.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akikagua daftari lenye orodha ya magari yaliyopimwa katika mzani wa Nkangamo katika barabara ya Tunduma-Sumbawanga(km 225) iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Wananchi wa Sumbawanga mjini wakifurahia hotuba ya Waziri wa Ujenzi kuhusu ujenzi wa barabara za lami mkoani Rukwa.
Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli akiwahutubia wananchi hao wa Sumbawanga mjini kuhusu ujenzi wa barabara za mkoa huo.
Sehemu ya barabara ya Tunduma-Sumbawanga km 225 iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami.
Waziri wa Ujenzi akiaagana na wakazi wa Sumbawanga mara baada ya kuwahutubia. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Wizara ya Ujenzi.

No comments:

Post a Comment