Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) akipokea hati ya
mradi wa mkongo wa mawasiliano nchini (Fiber Optic) toka kwa Ofisa Mkuu
wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge (kulia).
Mradi huo umeunganisha matawi ya benki ya TPB kimawasiliano ya kisasa.
Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (wa pili kulia) akizungumza
katika hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB
uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo
mbalimmbali nchini.
Mtatuzi wa Masuala ya Kiufundi, Fredrick Bernard akifafanua jambo
wakati wa hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB
uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 maeneo
mbalimmbali nchini. Hafla hiyo ilifanyika jana Makao Makuu ya TPB Dar es
Salaam.
Baadhi ya Maofisa wa TTCL wakiwa katika hafla ya makabidhiano ya mradi
mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani
matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.
Meneja Mkuu Uendeshaji wa TPB, Kolimba Tawa (kushoto) pamoja na Ofisa
Mkuu wa Ufundi wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Senzige Kisenge
wakipongezana kwenye hafla ya makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB
uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo
maeneo mbalimmbali nchini.
Picha ya pamoja ya maofisa wa TPB na TTCL walioshiriki katika hafla ya
makabidhiano ya mradi mpya wa benki ya TPB uliounganisha mawasiliano ya
kisasa takribani matawi 11 ya benki hiyo maeneo mbalimmbali nchini.
Na Mwandishi Wetu
BENKI ya Posta Tanzania (TPB) imedhamiria kuunganisha matawi yake yote
katika mfumo wa kisasa wa mawasiliano kupitia mkongo wa mawasiliano
nchini (Fiber Optic) ili kuberesha huduma na mawasiliano katika huduma
zake.
Taarifa
hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Meneja Mkuu Uendeshaji wa
TPB, Kolimba Tawa alipokuwa akizungumza katika makabidhiano ya mradi
mpya wa benki hiyo uliounganisha mawasiliano ya kisasa takribani matawi
11 maeneo mbalimmbali nchini.
Tawa
alisema mpaka sasa matawi ya Arusha, Mbeya, Mwanza, Dodoma, Samora,
Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo na Kijitonyama tayari yameunganishwa
kwenye mfumo huo mpya na wa kisasa kimawasiliano.
"..Mpaka
hivi sasa matawi yetu Kumi na Moja (11), yakiwemo Arusha, Mbeya,
Mwanza, Dodoma, Samora, Metropolitan, YWCA, Mkwepu, Ubungo, Kijitonyama,
tayari zimeunganishwa kwenye mfumo huo.
Hii
ni katika hatua ya mwanzo tu ya mradi huu, kwani benki ya Posta
imekusudia kuyaunganisa mtawi yake yote kwenye mfumo huu," alisema Tawa.
Alisema baada ya kukamilisha matawi ya TPB katika mfumo wa Mkongo (Fiber
Optic), imepata mafanikio makubwa ukilinganisha na kipindi cha nyuma
ambapo matawi haya yalikuwa yameunganishwa na mtandao wa teknolojia ya
Copper (Copper network).
Aidha
akizitaja faida ambazo benki hiyo imezipata baada ya kujiunga na Mkongo
wa Taifa wa Mawasiliano unaosimamiwa na kampuni ya Simu Tanzania (TTCL)
ni pamoja kupungua kwa msongamano wa wateja kusubiria huduma kwenye
matawi, kuongezeka kwa ufanisi na kupungua kwa dharura ya kusitisha
huduma kwa muda.
"...Pia
tumeboresha uwezekano wa kutambua tatizo lolote linalotokana na
kukatika kwa mawasiliano kwani huu ni mfumo wa kidijitali...kupungua kwa
gharama za uendeshaji katika benki yetu." alisema Tawa.
Kwa
upande wao TTCL ikikabidhi mradi huo kwa TPB, Mtatuzi wa Masuala ya
Kiufundi, Fredrick Bernard alisema mfumo huo wa mkongo unafaida kubwa
kwani, mbali na kuwa salama zaidi pia unauwezo wa kugundua tatizo la
mawasiliano kabla ya kutokea hivyo kufanyiwa kazi mapema.
Alisema
hata hivyo alisema njia za kupitisha mawasiliano hufanya kazi kwa
kutegemeana na zipo zaidi ya moja hali ambayo huwezesha hata njia moja
kuisaidia nyingine inapopata tatizo huku tatizo lililojitokeza
likishughulikiwa kwa wakati huo.
Faida
hizo pamoja na nyingine nyingi zinaifanya benki ya Posta iamini kuwa
huduma hii ya Mkongo itolewayo na TTCL ni bora nchini na itatusaidia
sana sisi benki ya Posta kuboresha huduma zetu na kuongeza ufanisi
katika shughuli zetu za kibenki.
No comments:
Post a Comment