Pages

February 3, 2015

Tigo kuwekeza dola millioni 30 za kimarekani katika kuboresha huduma zake kanda ya kaskazini mwaka 2015


Kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania, imedhamiria kuongeza uwekezaji katika mikoa ya kanda ya kaskazini kwa kiasi cha dola za kimarekani milioni 30.


Hayo, yamesemwa na Kaimu Meneja mkuu wa kampuni hiyo inayotajwa kuongoza kwa kuwa na wateja wengi kuliko kampuni nyingtine yoyote ya mawasiliano, Cecile Tiano(Pichani juu kulia) alipokuwa akiongea na waandishi wa habari mjini Arusha.

Tiano, aliyeteuliwa kushika nafasi hiyo mwezi huu, ameisifu kanda ya kaskazini inayojumuisha mikoa ya Arusha, Manyara, Singida, Dodoma na Kilimanjaro kuwa ni eneo la kibiashara na utalii bila kusahau kuwa ni njia kuu ya kuelekea mataifa jirani.


Alifafanua kwamba Tigo ina jumla ya minara 334 katika ukanda wa kaskazini ikiwemo 71 iliyojengwa mwaka 2014. Mwaka jana Tigo ilijenga jumla ya minara 312 nchi nzima.
 

“Mwaka huu tumepanga kujenga minara mingine 748 nchi nzima ambayo 300 itakuwa katika kanda ya kaskazini ili kuhakikisha wakazi wa vijiji vya mikoa yote mitano wanaunganishwa na huduma zetu. Kwa wastani wa dola 100,000 kila mnara, hii inamaanisha uwekezaji wa zaidi ya dola milioni 75 nchi nzima ikiwemo dola milioni 30 katika mikoa hii mitano.," Alisema.

“Hii inamaanisha watu wengi zaidi watapata fursa mpya za kijamii na kiuchumi, wakiunganishwa katika uchumi wa kidunia kupitia mtandao wa intaneti kwa kufanya hivyo tunawawezesha kujiunga na mfumo mpya wa digital,” alisisitiza Tiano.

Kanda ya Kaskazini pia imekuwa ikinufaika kwa kiasi kikubwa na mipango kadhaa ya udhamini na miradi ya kijamii kutoka Tigo, miradi ambayo Tiano alisema ina lengo la kuleta mageuzi chanya katika nyanja za elimu, afya, mazingira, ujasiriamali (ajira), sanaa na michezo.
 

“Kupitia juhudi zetu kama zile za mashindano ya Tigo Ngorongoro Run, mbio ambazo zimekuwa zikifanyika Karatu kila mwaka, kampuni yetu, pamoja na wadau wengine, tumeweza kukusanya fedha ambazo hutumika kununulia vyandarua shuleni, vifaa vya hospital imbalimbali katika wilaya ya Karatu,” alisema.

Katika hatua nyingine Tiano ametangaza udhamini wa Tigo kwa mbio za marathoni za Kilimnajaro mwaka huu kwa kiasi cha shilingi milioni 80. Mbio hizo zitafanyika tarehe 1 Machi 2015 ambapo Tigo inadhamini nusu marathoni ya kilomita 21


“Sababu ya Tigo kujiingiza katika mashindano haya ni kuonesha nia yake ya kuendeleza sekta ya michezo na nyanja nyingine za kijamii na za kiuchumi katika nchi hii, ikiwa ni pamoja na utunzaji wa mazingira", alifafanua Kaimu Meneja huyo

Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita Tigo imekuwa ikiwekeza kwenye miundombinu yake kwa wastani wa dola milioni mbili kwa wiki nchi nzima. Uwekezaji huu, kwa mujibu wa Tiano, umesaidia kupanua mtandao wake mpaka sehemu za vijijini na kuboresha mtandao wake hadi kufikia vipimo vya 3G hivyo kuwawezesha wateja kupata huduma ya Internet na kuelimisha wafanyakazi wake na kuleta manufaa kwa jamii kwa kuwekea katika miradi ya kijamii.


Tiano aliendelea kusema kuwa ndani ya miezi 12 iliyopita, Tigo imekuwa kampuni ya kwanza kubni huduma mpya zikiwemo kutuma na kupokea pesa kutoka Rwanda kupitia TigoPesa na kuanzisha huduma ya bure ya Facebook kwa Kiswahili pamoja na kuanzisha ushirikiano na kampuni nyingine za simu nchini kuwawezesha wateja kutuma au kupokea pesa kutoka mitandao hiyo.


Mafanikio mengine ni kuwawezesha wateja wake kuweke na kutoa pesa kutoka akaunti zao za benki kupitia simu zao za mkononi na kuwapa wateja gawio la faida itokanayo na utunzaji fedha zao katika akaunti zao za TigoPesa na na hivi karibuni uzinduzi wa huduma ya TigoMusic inayowapa wateja wake fursa ya kufurahia muziki bila kikomo kupitia Deezer.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...