Pages

February 1, 2015

PICHA ZA AJALI ILIYOTOKEA IRINGA NA KUUA WATATU NA PIKIPIKI KUWAKA MOTO

Hizi ndivyo lori hilo lilivyoharibika
WATU watatu waliokuwa wamepakizana mishikaki wamekufa kwa kuteketea kwa moto mjini Iringa usiku huu baada ya usafiri aina ya pikipiki (Boda boda)waliyokuwa wakisafiri kutoka mjini Iringa kuelekea Nduli nje kidogo na mji wa Iringa kugongana na lori aina ya Fuso na kupelekea pikipiki hiyo kuwaka moto.
Wananchi wakishuhudia ajali hiyo ya Lori na boda boda 

Hii ndio pikipiki iliyoteketea kwa moto baada ya ajali 
Ajali hiyo imetokea  wakati boda boda hiyo ikiwa katika mwendo mkali kugongana na lori hilo ambalo pia lilikuwa katika mwendo na kusababisha vifo hivyo . 
Mashuhuda wamesema kuwa kijana mmoja ambae inasadikika ndie dereva wa boda boda hiyo ametambuliwa kwa jina moja la Julius huku wengine wawili bado kutambuliwa . 
Kutokana na ajali hiyo mbali lori hilo upande wa mbele ngao yake ilipinda huku eneo hilo la mbele likiharibika vibaya mfano wa kugongana gari kwa gari na baada ya hapo pikipiki hiyo ilishika moto na kuteketea yote pamoja na watu hao ambao miili yao ilizimwa kwa mchanga na wasamaria wema.
Miili ya marehemu hayo imehifadhiwa katika chumba cha maiti cha Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa utambuzi zaidi

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...