Pages

February 10, 2015

NAPE: HAKUNA MGOMBEA ATAKAYEPITISHWA CCM KWA PRESHA ZA MAKUNDI, NI KWA KUKIDHI VIGEZO VYA KANUNI NA KATIBA ZA CHAMA TU


NA BASHIR NKOROMO.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesema, hakuna kitakayempitisha kugombea urais 2015, kwa presha za makundi au wapambe.

Akizungumza kwa nyakati tofauti katika vyumba vya habari vya magazeti ya Habari Corporation, na Mwananchi Communication Ltd, jijini Dar es Salaam, leo, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema, mfumo wa CCM katika kuwapata wagombea ni imara kiasi kwamba hautaweza kuathiriwa na presha za makundi wakati wa kuteua mgombea urais katika uchaguzi mkuu mwaka huu.

Amesema, ni vigezo vinavyozingatia kanuni na katiba ya Chama tu ndivyo vitakavyomuwezesha anayetaka kupeperusha bendera ya CCM kupitishwa na Chama, vinginevyo haitawezekana hata kama ana makundi yenye presha kiasi gani.

"Chama hiki kina mfumo na taratibu ambazo haziwezi kusukumwa na presha za wapambe wa mgombea yeyote, na hata kumbukumbu zinaonyesha kwamba katika chaguzi zilizopita, wamewahi kuwepo wagombea wenye makundi yenye presha kiasi cha kudhaniwa ndio wangeteuliwa, lakini baada ya kufika mbele ya taratibu na kanuni waliachwa na nafasi kupewa wengine", alisema Nape.

Alisema, kanuni na taratibu ndizo mwamuzi wa mwisho katika kuteua wagombea wa CCM, "Sisi tukisema wanaotaka nafasi hii njooni mjipime hapa, mmojawapo akijaiona hatoshi lakini kwa ujanja akaongeza matofali kupata urefu... huyo taratibu zitatumia kuondoa matofali ili abaki kama alivyo kuona kama anatosha", alisema Nape.

"Na katika utaratibu huu wa kuondoa matofali ndiyo watajitokeza baadhi yao kulalamika kwa sababu itauma kidogo", alisema.
HABARI KATIKA PICHA
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akiingia katika ofisi za Kampuni ya Habari Corporation Ltd, kendelea na ziara katika vyombo vya habari aliyoianza wiki iliyopita. Kushoto ni Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Umma wa CCM, Godfrey Chongolo
 Nape akisalimiana na Mhariri Mkuu wa Habari Corporation Denis Msaky baada ya kuingia chumba cha habari
 Nape akisalimiana na Matinyi ambaye ni mmoja wa wahariri katika kampuni hiyo ya Habari Corporation, wachapishaji wa magazeti ya Mtanzania, Rai na Dimba
 Napa kisalimiana na Mhariri wa Msanifu wa Habari wa Mtanzania Hamis Mkotya.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...