Pages

February 4, 2015

NAIBU WAZIRI WA NISHATI AKUTANA NA UJUMBE WA WAFANYABIASHARA KUTOKA UJERUMANI

Katibu wa Nchi kutoka Wizara  inayohusika na Masuala ya Uchumi na Nishati ya Ujerumani  Mattias Machnig (kulia) akisisitiza jambo katika kikao kilichokutanisha ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani na  Naibu  Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga kwa ajili ya kujifunza fursa za uwekezaji katika sekta za nishati na madini nchini.

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Charles Kitwanga na Kaimu  Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava pamoja na ujumbe wa wafanyabiashara kutoka nchini Ujerumani  wakifuatilia kwa makini maelezo yaliyokuwa yanatolewa na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia masuala  ya umeme, Mhandisi Innocent Luoga ( aliyekaa mbele wa kwanza kushoto) juu ya  fursa za uwekezaji katika  sekta ndogo ya umeme.

No comments:

Post a Comment