Pages

February 16, 2015

Muendelezo wa maisha ya OSCAR PISTORIUS gerezani South Africa

image

Mwanariadha Oscar Pistorius ambaye anatumikia kifungo kwa baada ya Mahakama Afrika Kusini kumkuta na hatia ya mauaji ya aliyekuwa mpenzi wake, Reeva Steenkamp kwa kumpiga risasi ndani ya nyumba yake leo kuna taarifa ya muendelezo wa kinachoendelea gerezani.
Kwa utaratibu wa Magereza Afrika Kusini wanapanga wafungwa kwa madaraja tofauti,Pistorious alikuwa ‘Category B’ lakini kwa sasa yuko ‘Category A’, hapa alipo sasa anaruhusiwa kukutana na wageni wowote wanaomtembelea mbali na ilivyokuwa mara ya kwanza ambapo alitakiwa akutane na ndugu zake tu.
Kwa sasa anaweza pia kusikiliza Radio, kuvaa vitu vya thamani kama cheni, pete.
Msemaji wa familia yake Annalise Burgess amesema mwanariadha huyo kwa sasa amepandishwa hadhi na kuwa ‘Category A’, anaweza kupiga simu na kununua vyakula anavyotaka.
pistorius9
Suala la Oscar kupandishwa daraja limewakera wafungwa wenzie walioko kwenye gereza la Death Island, ambao wamelalamika kuwa mwanariadha huyo anapewa hadhi  hiyo ndani ya kipindi cha muda mfupi wakati wao wamekaa muda mrefu gerezani na hawajapata hadhi hiyo.
Pistorius alihukumiwa kifungo cha miaka mitano jela mwaka jana mwezi August.

No comments:

Post a Comment