Matumizi ya mitandao ya kijamii
yameshusha utu wa watu ikiwa ni pamoja na kujikuta nidhamu inakuwa mbaya
kwa baadhi ya watu wenye kueshimiwa na jamii. STEVEN WASIRA Ni kiongozi
wa serikali ya Tanzania ambae Ni BABA kwa walio wengi hususani kwa wale
ambao wametumia picha yake na kuisambaza katika mitandao ya kijamii
ikiwemo FACEBOOK na WHATS AP
Napenda kuuliza swali kwa Watanzania
wenzangu, Jee kinachoendelea kwa sasa katika mitandao ni cha manufaa kwa
jamii au ni kujishusushia heshimaa!!!!!!!!!!!
Katika picha hizi hapa hawa ni baadhi ya
watu wenye akili na wadhifa mbalimbali katika nchi ya Tanzania .
Kwa muonekano hawa ni wafanya kazi wa taasisi inahifadhiwa nao wanasherekea baba yao kuvaa nguo vibaya wanaamini ya kwamba wao ni bora zaidi
Kwa wadhifa wake huyu ni daktari ambae ana taaluma
yake lakini mwisho wa mawazo yake ndio huo
Huyu nae ni mzee mwenye umri sawa na Wasira lakini nae ameona ni vema kumpuuza mzee mwenzake kwa kusambaza picha zake akiwa katika hali hiyo..
Sasa swali linakuwa hivi,,, Endapo STEVIN WASIRA angekuwa baba yao bado wangefanya hivyooo
Watanzania tuwe makini jamani tuendako tutakuja tuwapige wazazi wetu picha wakiwa katika mazingira tatanishi na kuzisambaza katika mitandao ya kijamii ..
Mitandao ya kijamii ni moja kati ya nguzo kubwa ya mafanikio lakini endapo tutazidi kuitumia kwa mambo yasiyo na tija huenda tukazidi kurudi nyuma kimaendeleo tofauti na ilivyo lengo la SOCIAL NERWORCK..
No comments:
Post a Comment