Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma
Kikwete akiangalia ngoma za utamaduni mara baada ya kuwasili kwenye
sherehe za kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti (Mammograph)
kwa akinamama katika Hospitali ya Jeshi Lugalo kwenye kitengo cha Uzazi
na mtoto kilichopo eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015. Aliyesimama
kushoto kwa Mama Salma ni Luteni Jenerali Samuel Ndomba, Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel
Ndomba akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupima
saratani ya matiti kwa akina mama katika Hospitali ya Lugalo
Baadhi
ya viongozi wa Jeshi la Ulinzi na wananchi waalikwa wakisikiliza kwa
makini hotuba ya mgeni Rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa hafla ya
kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama.
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma
Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya
kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi
Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha
hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar .
Mnadhimu
Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel
Ndomba akimpongeza Mama Salma Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye
hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama
kwenye hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo .
Mke wa
Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya
kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu
wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia).
Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi
Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge . Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal
Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika
mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini
hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha
Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya
matiti kwa akina mama .
Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi
wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza
baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama
Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki.
PICHA NA JOHN LUKUWI
No comments:
Post a Comment