Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais Edgar Lungu wa Zambia
wakigonga glasi wakati wa dhifa ya kitaifa aliyoiandaa kwa heshima ya
Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.
Rais
Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akigonga glasi na Rais wa Kwanza wa taifa la
Zambia Dkt.Kenneth Kaunda wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa
heshima ya Rais Kikwete jijini Lusaka Zambia jana jioni.Rais Kikwete
ambaye alikuwa katika ziara ya siku mbili nchini Zambia tayari amerejea
jijini Dar es Salaam.
Dkt.Jakaya
Mrisho Kikwete na mwenyeji wake Rais wa Zambia Edgar Lungu pamoja na
wake zao Mama Salma Kikwete na Mama Esther Lungu wakinyanyua glasi juu
wakati wa dhifa ya kitaifa iliyoandaliwa kwa heshima ya Rais Kikwete na
ujumbe wake ambao walifanya ziara ya kikazi ya siku mbili nchini Zambia.
.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Rais wa kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth David Kaunda nyumbani kwake Mkango Barracks,State lodge, nje ya jiji la Lusaka leo.
Rais wa Kwanza wa Zambia Dkt.Kenneth Kaunda akimpa zawadi Rais Dkt.Jakaya Kikwete
Rais
Dkt.Jakaya Kikwete akisindikizwa na Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee
Kenneth Kaunda mara baada ya kumtembelea na kufanya naye mazungumzo leo
Rais
Dkt.Jakaya Kikwete akiagana na Rais wa Kwanza wa Zambia Mzee Kenneth
Kaunda mara baada ya kumtembelea na kufanya naye mazungumzo leo Picha na
Freddy Maro
No comments:
Post a Comment