Pages

February 23, 2015

JAJI AUGUSTINO RAMADHANI AKUTANA NA MWAKILISHI WA "FRANCOPHONIE" ARUSHA LEO

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino Ramadhani(kushoto) akiwa kwenye mazungumzo na  Naibu Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa  “La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis Ababa,Ethiopia,Cecile Folchini  kwenye ofisi za Mahakama ya Afrika jijini Arusha leo.

 Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino Ramadhani(wa pili kulia)akiwa katika picha ya pamoja na  Naibu Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa  “La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis Ababa,Ethiopia,Cecile Leque Folchini(kulia)kushoto ni Msajili wa mahakama hiyo,Dk Eno Robert na Mkurugenzi wa Alliance Francaise d'Arusha,Gaelle Lapostolle.


 Mwandishi Wetu

Rais wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu(AfCHPR)Jaji Augustino Ramadhani leo amefanya mazungumzo na  Naibu Mwakilishi Mkazi wa taasisi ya kimataifa  ya “La Francophonie” katika Umoja wa Afrika(AU)yenye makao yake Addis Ababa,Ethiopia,Cecile Folchini  kwenye ofisi za Mahakama ya Afrika jijini Arusha ambayo yamejikita kushirikiana baina ya taasisi hizo mbili.

Cecile alisema taasisi yake iko mbioni kuona ni namna gani wataisaidia Mahakama hiyo ya Afrika ya Haki za Binadamu ili kuiwezesha kufanya kazi zake ipasavyo.

Katika ujumbe wake aliambatana na Mkurugenzi wa Alliance Francaise d'Arusha,Gaelle Lapostolle ambayo hutoa mafunzo ya kifaransa ambayo iliahidi kutoa mafunzo kwa Majaji wa Mahakama hiyo kujifunza kifaransa katika muda wao wa ziada.

Mahakama hiyo ina Majaji kutoka nchi mbalimbali zikiwemo zisizotumia lugha ya kifaransa kama lugha rasmi zikiwemo Afrika Kusini,Tanzania,Uganda,Malawi na Kenya.

Lugha rasmi za Mahakama hiyo ni Kiingereza,Kifaransa,Kireno na Kiarabu.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...