Pages

January 8, 2015

WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AZINDUA MRADI MKUBWA WA REA WA SHILINGI BILIONI 25.7 MKOANI SIMIYU

Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo leo amezindua mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili, mkoani Simiyu ambapo vijiji 170 vimeunganishwa na mradi huo. Ninawasilisha picha za matukio pamoja na captions kwa ajili ya kuchapishwa kwenye vyombo vyenu vya habari ili kuhabarisha umma. Aidha, captions zinapatikana mwishoni mwa email hii.
Mwananchi kutoka katika kijiji cha Nyanguge kilichopo wilayani Bariadi mkoani Simiyu akiwasilisha hoja mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo ( wa kwanza kulia) mara Waziri alipotembelea kijiji hicho wakati akielekea kwenye uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) Awamu ya Pili wenye thamani ya shilingi bilioni 25.7.
Mkuu wa Wilaya ya Bariadi Erasto Sima akizungumza na wanakijiji wa Nyanguge wilayani Bariadi juu ya utunzaji wa miundombinu ya umeme iliyowekwa na REA. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Sehemu ya umati wa watu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu.
Sehemu ya watoto kutoka katika kijiji cha Shishiyu kilichopo wilayani Maswa mkoani Simiyu waliojitokeza kushuhudia uzinduzi wa mradi wa umeme uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili.
Wananchi wa kata ya Shishiyu wakinyanyua mikono juu kama ishara ya kuridhishwa na utekelezaji wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo akihutubia wananchi wa kata ya Shishiyu (hawapo pichani) kabla ya kuzindua rasmi mradi wa umeme.
Mtaalamu kutoka kampuni ya LTL (PVT) LTD Michael Marenye akitaja orodha ya vijiji vilivyonufaika na mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo.
Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda akimpongeza Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa kazi kubwa aliyoifanya ya kusambaza umeme katika jimbo lake.
Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto) akitafsiri hotuba ya shukrani iliyotolewa kwa lugha ya kisukuma na mmoja wa wakazi wa kijiji cha Shishiyu mbele ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kabla ya kuzinduliwa rasmi kwa mradi huo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akikata utepe kama ishara ya uzinduzi wa mradi wa umeme vijijini uliotekelezwa na REA Awamu ya Pili.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (mwenye tisheti ya kijani) akisoma maandishi kwenye jiwe la msingi mara baada kukata utepe kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati) Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (kushoto mwa Waziri) na mmoja wa wakazi wa Shishiyu wakibonyeza kitufe kama ishara ya uzinduzi wa mradi huo.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (katikati aliyeshika mtoto); Mbunge wa Maswa Magharibi John Magale Shibuda (wa pili kutoka kulia waliokaa mbele) na Diwani wa Kata ya Shishiyu wilayani Maswa Pili Kidesela (wa kwanza kulia waliokaa mbele) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watendaji wa Shirika la Umeme Nchini (Tanesco) mara baada ya kumalizika rasmi kwa uzinduzi wa mradi huo.

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...