Pages

January 15, 2015

WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (KAZI MAALUM), MHESHIMIWA PROF. MARK MWANDOSYA AFANYA ZIARA YA KIKAZI NCHINI SUDANI

New Picture (1) 
Mhe. Prof. Mark Mwandosya akifafanua jambo wakati wa mkutano wa pamoja na Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Bwana Felix Ngamlagosi ambaye ameongozana pamoja na maafisa wengine na Waziri Prof. Mwandosya
New Picture (2) 
Mhe. Prof. Mark Mwandosya akitoa maelezo katika mkutano wa pamoja na Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim.
New Picture (3) 
Ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Mhe. Prof. Mark Mwandosya katika mkutano wa pamoja na ujumbe wa Sudan ulioongozwa na Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe Mutaz Moussa Abdallah Salim.
New Picture 
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Mhe. Prof. Mark Mwandosya akikaribishwa na mwenyeji wake Waziri wa Maji na Umeme wa Sudan Mhe. Mutaz Moussa Abdallah Salim mara alipowasili katika Ofisi za Wizara hiyo Jijini Khartoum.
……………………………………………………………………………………………………………………………………..
12 – 17 JANUARI 2015 Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Mark Mwandosya yuko ziarani nchini Sudan ambako atatembelea miradi mbalimbali ya maendeleo nchini humo ikiwemo miradi mikubwa ya mabwawa yaliyojengwa katika bonde la Mto Nile pamoja na kubadilishana uzoefu na taasisi za Sudan zinazojihusisha na udhibiti wa huduma katika sekta za maji, nishati, mawasiliano na usafirishaji.

Ujumbe wa Mhe. Prof. Mwandosya umejumuisha wataalamu kutoka Wizara ya Maji, Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA) na Mamlaka ya Mawasiliano (TCRA).

Mhe. Prof. Mwandosya alianza ziara yake Jumatatu ya tarehe 12 Januari, 2015 kwa kutembelea Wizara ya Rasilimali za Maji na Nishati ya Umeme ya Jamhuri ya Sudan. 
  Katika ziara hiyo Mhe. Prof. Mwandosya alieleza kuwa pamoja na shughuli zingine, ameandamana na taasisi za udhibiti kutoka Tanzania ili kujifunza na kubalishana uzoefu katika shughuli za udhibiti kutoka kwa taasisi kama hizo katika nchi ya Sudan. 

Waziri alieleza kuwa shughuli za udhibiti Tanzania zimekuwa zikifanyika kwa kipindi cha takribani miaka 10 sasa. Waziri alieleza kuwa pamoja na mafanikio yaliyopatika katika kutekeleza majukumu yao, Mamlaka za Udhibiti bado zina changamoto nyingi ambazo inabidi kukabiliana nazo kwa kujifunza na kubadilisha uzoefu na taasisi kama hizo katika nchi kama Sudan.

No comments:

Post a Comment