Pages

January 10, 2015

WAZIRI MKUU AHITIMISHA ZIARA YAKE WILAYANI MPANDA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na viongozi wa mkoa wa Katavi kwenye uwanja wa ndege wa Mpanda baada ya ziara yake ya jimbo la uchaguzi Januari 9, 2015. Kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda, Pazi Mwamlima, Katibu Tawala wa Mkoa wa Katavi, Mhandisi Emmanuel Kalobelo na Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Kanali Ngemera Lugunga.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiangalia msokoto wa rasta isiyokuwa ya kawaida aliosuka Bwana huyo, baada ya kuwasili kwenye uwanja wa shule ya ufundi ya Mamba wilayani Mlele kuhutubia mkutano wa hadhara Januari 9, 2015. 
Sungusungu wa tarafa ya Mamba wilayani Mlele wakicheza ngoma wakati Mbunge wao, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipowasili kwenye uwanja wa Shule ya Ufundi ya Mamba kuhutubia Mkutano wa hadhara Januari 9, 2015.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments:

Post a Comment