Msanii Wastara akiwa kainama kwenye kaburi la marehemu mumewe Sajuki.
Marehemu Sajuki alifariki dunia Januari 2.2013 , ambapo leo ametimiza
miaka miwili, dua ya kumuombea ilianzia katika makaburi ya Kisutu,
jijini Dar es Salaam ambapo marehemu Sajuki alizikwa na baadae kuhamia
nyumbani kwake Tabata.
Akizungumza na GPL, Wastara alisema anajisikia faraja sana kusoma dua
kwa ajili ya mtu aliyempenda lakini pia anawashukuru wadau na wote
waliojitokeza katika kufanikisha kisomo hicho.
Aidha wasanii mbalimbali wamejitokeza akiwemo Mohamed Mwikonge
‘’Frank’ Mtitu, Nisha, Bond na wengineo ambao pia wameomba na
kuwakumbusha wasanii na wadau mbalimbali kuwakumbuka na kuwaenzi wasanii
pindi wanapoaga dunia

Post a Comment