Mamlaka
ya Mapato nchini (TRA) imetoa semina juu ya Himaya Moja ya Forodha
(Single Customs Territory) kwa watumishi na viongozi waandamizi wa Ofisi
ya Rais, Tume ya Mipango.
Akizungumza
katika ufunguzi wa Semina hiyo, Naibu Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais,
Tume ya Mipango na Mkuu wa Kongane ya Biashara ya Kimataifa na
Ushirikiano wa Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe amesema kuwa semina hiyo ina
lengo la kuhakikisha kuwa kuna uelewa wa pamoja kuhusu utaratibu huo kwa
watumishi wa umma na watanzania wote.
“Lengo
la semina hii ni kupata ufahamu wa kutosha kuhusu mambo mbalimbali
yanayoendelea, ili kuweza kushauri Serikali ipasavyo katika masuala
mbalimbali ya kisera katika Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki,” alisema Bw. Sangawe.
Akiwasilisha
mada juu ya Mfumo wa Himaya Moja ya Forodha kwa watumishi, Mtaalamu wa
Masuala ya Forodha, Bw. Stambuli Myovela alisema kwamba mfumo huo
unaainisha utaratibu wa Mzunguko Huru wa Biashara, Usimamizi wa Mapato,
na Mfumo wa Kisheria.
Bw.
Myovela aliongeza kuwa kwa mujibu ya mfumo uliokubalika ni kwa kila Nchi
Wanachama zitakushanya mapato yake ya kodi. Aidha, kwa bidhaa
zinazopitia Nchi moja kuelekea katika Nchi nyingine wanachama (Transit
Goods), Nchi Wanachama zimekubaliana kuwa nchi husika bidhaa
zinapokwenda itakusanya mapato yake na kuifahamisha mamlaka ya forodha
mizigo ilipoingilia katika Jumuiya kwa ajili ya kuruhusu bidhaa
kuondoshwa.
Akieleza
namna ya utendaji kazi wa mfumo huo, Bw. Myovela aliongeza: “Baada ya
kuthibitisha kuwa kodi imelipwa, mizigo itasafirishwa kutoka kituo cha
kwanza cha forodha chini ya usimamizi wa Mamlaka ya Forodha kwenda nchi
ambayo mizigo hiyo imekusudiwa kutumika ndani ya Jumuiya. Mfumo maalum
wa ufuatiliaji kielektroniki (Electronic Cargo Tracking System)
utatumika kuhakikisha mizigo inafika salama katika nchi iliyokusudiwa
katika Jumuiya.”
Mfumo
wa Himaya Moja ya forodha uliridhiwa na Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya
Afrika Mashariki katika Mkutano wake wa 28 ambapo kwa pamoja Mawaziri
hao waliridhia kuwa na Mpangokazi unaoainisha masuala ya kutekeleza
katika kipindi cha miezi sita ili kuwezesha kuanzishwa kwa Himaya Moja
ya Forodha ifikapo mweizi Juni, 2014.
Naibu
Katibu Mtendaji wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango na Mkuu wa Kongane ya
Biashara ya Kimataifa na Ushirikiano wa Kiuchumi, Bw. Paul Sangawe
(Kushoto) akizungumza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Himaya Moja ya
Forodha (Single Customs Territory).
Mtaalamu
wa Masuala ya Forodha kutoka TRA, Bw. Stambuli Myovela (Kulia)
akizungumza wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs
Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Baadhi
ya watumishi wataalamu wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango wakifuatilia
kwa umakini mawasilisho kuhusu Himaya Moja ya Forodha (Single Customs
Territory) katika semina iliyoandaliwa na Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA).
Mtaalamu
wa Masuala ya Forodha kutoka TRA, Bw. Stambuli Myovela (aliyesimamaa)
akifanya mawasilisho juu ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs
Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Naibu
Katibu Mtendaji (Huduma za Jamii na Masuala ya Idadi ya Watu), Ofisi ya
Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kushoto) akichangia mada
wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs Territory)
kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mchumi
Mkuu kutoka Kongane la Uchumi Jumla, Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango,
Bibi Salome Kingdom (Kushoto) akiuliza swali kuhusu Himaya Moja ya
Forodha (Single Customs Territory).
Bw.
Elykedo Ngonyani ambaye ni Mchumi Mwandamizi (Sekta za Uzalishaji)
akichangia mada wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single
Customs Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
Mtaalamu
wa TRA anayeratibu masuala ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs
Territory), Bi Leah Skauki akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati
wa wakati wa Semina ya Himaya Moja ya Forodha (Single Customs
Territory) kwa watumishi wa Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango.
No comments:
Post a Comment