Pages

January 14, 2015

TANZANIA YASHIRIKI KATIKA MKUTANO WA KUMI WA MAENDELEO YA TAKWIMU AFRIKA NCHINI UGANDA.

 Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akiwahutubia washiriki mbalimbali kutoka barani Afrika (hawapo pichani) wakati wa Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyonyo Kampala, Uganda. 
 Washiriki kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.  Kushoto ni Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika Prof. Innocent Ngalinda, katikati ni Meneja wa Takwimu za Kilimo Titus Mwisomba kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu na kulia ni Mwenyekiti wa  Bodi ya Ofisi ya Taifa ya Takwimu Prof. Milline Mbonile.
 Washiriki wengine kutoka Tanzania wakisikiliza kwa makini mambo yanayoendelea katika Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika leo katika Ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyonyo Kampala, Uganda. Kushoto ni Meneja wa Sensa ya Watu na Makazi Irenius Ruyobya akifuatiwa na Dkt. Camilius Kasalla kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.
  Waziri Mkuu wa Uganda Mhe. Ruhakana Rugunda akimpongeza Mwandishi wa Kitabu cha Mapinduzi ya Takwimu Afrika Prof. Ben Kiregyera baada ya kukizindua leo kwenye Mkutano wa Kumi wa Maendeleo ya Takwimu Afrika uliofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Speke Munyoyo Kampala, Uganda.  (PICHA NA VERONICA KAZIMOTO - KAMPALA)

No comments:

Post a Comment