Mmoja wa majeruhi wa shambulio la leo akipatiwa huduma ya kwanza na kikosi cha uokoaji.
POLISI
mmoja wa kike ameuawa kwa risasi huku wafagiaji wa mitaani wakijeruhiwa
baada ya kushambuliwa na mtu aliyekuwa na silaha katika shambulio la
pili ndani ya saa 24 lililotokea eneo la Montrouge jijini Paris nchini
Ufaransa.
Shambulio
la leo limetokea kusini mwa mji wa Paris huku mshambuliaji aliyekuwa
amaevaa nguo ya kuzuia risasi 'bullet prof' akitumia silaha aina ya M5.
Polisi huyo alisimaa mtaani kukagua ajali iliyotokea barabarani kabla ya kushambuliwa na mtu huyo.
Shuhuda wa shambulio hilo anadai kusikia milio ya risasi tano kwenye tukio hilo.
Shambulio
hilo limetokea ndani ya saa 24 baada ya shambulio la jana katika ofisi
za magazeti ya vikatuni ya Charlie Hebdo jijini Paris, Ufaransa lililoua
watu 12 na kujeruhi kadhaa. Bado haijafahamika kama shambulio la leo
lina uhusiano wowote na lile la jana.
No comments:
Post a Comment