Mratibu
wa kituo cha TFGM na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Mtakatifu Catherine
Laboure ya Kijiji cha Masanga kilichopo wilayani Tarime mkoani Mara,
Thomas Maruga akiwatembeza maeneo mbalimbali ya shule hiyo na Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
watu duniani (UNFPA), Dkt. Natalia Kanem (kushoto) wakati wa sherehe ya
mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji (Waiseke
wa Kisasa).(Picha za Zainul Mzige wa MOblog)
.
Na Mwandishi wetu, Tarime-Mara
SERIKALI imeombwa kuhakikisha inakomesha ubabe unaotumika kukeketa mabinti wa koo za Kikuria nchini.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha
Masanga, Tarime Sista Germaine Baibika akizungumza na waandishi wa
habari baada ya kukamilika kwa sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti
waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
Alisema
jumla ya mabinti 634 wamehitimu mafunzo ya miezi miwili yanayogusa haki
za binadamu, haki zao, masuala ya afya na kuzitambua na kuezinzi mila
nzuri.
Aidha wamejifunza kazi za sanaa na usanii.
Alisema
adha kubwa wanayokumbana nayo mabinti hao waliotoka katika kituo hicho
ni kukamatwa kwa nguvu na kupitishwa kisu cha Ngariba bila wao wenyewe
kuafiki kwa dai la kuendeleza mila.
“Hii
sio mila” anasema sista Germaine na kuongeza kuwa hakuna mila
inayotengenezwa kunyanyasa watu wengine au kulazimisha mambo yasiyofaa
katika jamii, mila hiyo ikiwepo lazima ipigwe vita.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kazi na Ajira, Mh. Gaudentia Kabaka (wa pili kushoto)
akiwasili kwenye mahafali hayo pamoja na Mratibu Mkazi wa mashirika ya
Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kushoto) aliyeambatana na
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem.
Alisema
serikali isiache kuwatetea mabinti hao kwa dai la kuwa hiyo ni mila kwa
kuwa wanaofanyiwa vitendo hivyo hulazimishwa na haifanyiki kwa ridhaa
yao.
Alisema
wapo mabinti walioletwa na wazazi wao kuepushwa na janga hilo, wapo
waliotoroka kwa wazazi wao na wapo walioletwa katika kituo hicho na
polisi kutoka makwao.
Mafunzo
hayo ya mwezi mmoja yamelenga kukabiliana na msimu wa ukeketaji ambao
sisita huyo alisema mwaka jana ulianza mapema Novemba na unaendelea hadi
mwaka huu wakati kimila mwaka huu si wa ukeketaji.
Kwa mujibu wa mila za Kikuria ukeketaji hufanyika katika mwaka unaogawanyika, mwaka 2015 haugawanyiki.
Mhashamu
Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara, Michael
Msongazila akiwasili kwenye sherehe za mahafali ya sita ya kituo cha
kupambana na ukeketaji Masanga wilayani Tarime mkoani Mara.
Mafunzo
hayo ambayo yamelenga kuwatoa mabinti wa kisasa wenye mwelekeo wa
maisha yenye hali bora mabinti wanaofika hapo huwa hawataki kukeketwa na
ndio maana mwaka huu walipata tatizo la binti mmoja kuzimia wakati
alipomuona baba yake katika maeneo ya kituo hicho.
Alisema
wapo wazazi wakorofi wanaokuja kudai watoto wao lakini pia ipo jamii
korofi inayotumia ubabe baada ya wasichana hao kutoka hapo wanakeketwa
kwa lazima.
Katika
hafla hiyo iliyoendeshwa na masista wa shirika la Daughters of Charity
of St. Vincent De Paul, Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka
aliwapongeza wasichana hao na kuwataka kuwa mfano katika jamii na
kutekeleza wajibu wao.
Alisema wamekuwa mabinti wa kisasa kwa kukataa ukeketaji na hivyo wao wanastahili kuwa walimu kwa wenzao.
Maandamano
ya wanafunzi wa Shule ya Mtakatifu Catherine Laboure iliyopo kijiji cha
Masanga wilayani Tarime, mkoani Mara wakiwa na mabango yenye jumbe
mbalimbali za kukemea ukeketeji wakisindikiza dada zao wahitimu wa kituo
cha FGMT katika sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti (Waiseke wa
kisasa) waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji yaliyofanyika mwanzoni mwa
wiki.
Aidha
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez
amewataka mabinti hao kuwa chachu ya mabadiliko katika jamii na kuwa
chanzo cha kubadili kizazi kijacho.
Alisema wamesimama madhubuti kupinga mila potofu na uonevu na kusema kwa kitendo chao wamewafanya wengine kuwaiga na kubadilika.
Alisema
ukeketaji ni mila potofu na kusema kwa msaada wa shirika la Umoja wa
mataifa la Mpango wa familia (UNFPA) na taasisi nyingine zinazopambana
na ukeketaji kwa kipindi cha miaka saba wamefanikiwa kuwoakoa wasichana
2001 wasikeketwe.
Aidha mabinti hao wameokolewa dhidi ya ndoa za utotoni, ujauzito wa mapema na kushindwa kuendelea na masomo.
Naye
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
watu duniani (UNFPA), Dkt Natalia Kanem amesema ni vyema mapambano dhidi
ya ukeketaji yakaendelea kwa kuwa wanaoshabikia ni viongozi wa kimila
na ngumu kuiondoa ila kwa juhudi za jamii yenyewe.
Katika
sherehe hizo ambapo pia askofu wa Musoma alikuwepo na viongozi
wengine wa kiserikali pia Ngariba walioacha kazi hiyo walikuwepo
kuelezea ubaya wa mila hiyo.
Suala la ukeketaji ni kitu cha kawaida katika mikoa ya Manyara 71%, Dodoma 64%, Arusha 57%, Singida 51% na Mara 40%.
Viongozi
waliopata muda wa kuzungumza walisema kwamba ukeketaji unatakiwa
kukomeshwa mara moja kwani ni tatizo si tu kwa jamii bali kwa wale
ambao wanafanyiwa kisaikolojia na kitabibu.
Wahitimu
mabinti 37 waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji wa kituo cha TFGM cha
kijiji cha Masanga wakiwasili na maandamano kwenye sherehe za mahafali
ya sita ya kituo hicho.
Moja
ya kazi inayoifanywa na kituo cha Masanga ni ushauri wa kisaikolojia
kutokana na wasichana wengi kufika hapo wakiwa na matatizo makubwa ya
magonjwa na hasa msongo wa mawazo.
Katika
risala yao mabinti hao wameitaka serikali kufanyakazi yake kukabiliana
na ubabe unaofanywa na viongozi wa kimila wa kuwalazimisha kukeketwa
hata msimu unapokuwa umepita.
Mabinti
hao ambao wengi wametoka shule ya msingi na sekondari wameweza kuwekwa
hapo kwa msaada wa UNFPA ambao wametoa hela kupitia Children’s Dignity
Fund (CDF), .Wafadhili wengine ni Daughters of Charity of St. Vincent Du
Paul, na Askofu wa kanisa katoliki dayosisi ya Musoma, Michael
Msongazila
Mgeni
rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akisalimiana na
Mhashamu Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Mkoani Mara,
Michael Msongazila mara baada ya kuwasili kwenye mahafali hayo.
Kwaya
ya vijana ya mara ikiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuanza kwa sherehe za
mahafali ya sita ya kituo cha kupambana na ukeketaji Masanga wilayani
Tarime mkoani Mara.
Mgeni
rasmi Mh. Kabaka, Bw. Alvaro Rodriguez na SSP. Simon Mrashani
wakishiriki kucheza wimbo maalum unaohamasisha kukataza vitendo vya uovu
vya Ukeketaji kwa watoto wa kike wakati wa mahafali hayo.
Meza kuu ikitoa heshima kwa wimbo wa taifa.
Mkurugenzi
wa Kituo cha kupambana na ukeketaji cha Masanga (TFGM), Tarime, mkoani
Mara, Sista Germaine Baibika akimkaribisha mgeni rasmi pamoja wageni
waalikwa kwenye sherehe ya mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa
msimu wa ukeketaji.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akifurahi jambo na
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez kwenye
sherehe za mahafali hayo.
Mgeni
rasmi Waziri wa Kazi na Ajira Mh. Gaudentia Kabaka akizungumza kwenye
sherehe za mahafali ya sita ya mabinti waliokwepeshwa msimu wa
ukeketaji.
Mratibu
Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa
salamu za Umoja wa Mataifa katika sherehe za mahafali sita ya mabinti
waliokwepeshwa msimu wa ukeketaji.
Mkuu
wa Wilaya ya Tarime, mkoani Mara, Bw. John Henjewele akitoa salamu kwa
niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika mahafali ya sita ya kituo cha
kupambana na ukeketaji cha kijiji cha Masanga (TFGM) cha wilayani
Tarime, mkoani Mara.
Mwakilishi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya watu duniani
(UNFPA), Dkt Natalia Kanem, akizungumza kwenye sherehe hizo.
Kaimu
kamanda wa polisi wa kanda maalum ya Tarime na Rorya SSP. Simon
Mrashani akieleza jinsi jeshi la polisi linavyoshiriki katika kupambana
na masuala ya unyanyasaji wa kijinsia likiwemo suala la kesi za
ukeketaji ambapo pia alitoa takwimu za kesi zilizoripotiwa kituoni mpaka
sasa ni 141, huku 80 zikiwa Mahakamani na 20 zimetolewa hukumu.
Mtaalam
wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce
Temu akifurahi jambo na baadhi ya wafanyakazi wenzake wakati wa sherehe
za mahafali hayo.
Wahitimu
37 wakila kiapo cha kutokubali kutoshiriki kukeketwa na kuwa mabalozi
wazuri kwenye jamii zao katika kuelemisha madhara ya ukeketaji kwa
wanaoendeleza mila na tamaduni hizo pindi warudipo majumbani. Kwa picha zaidi ingia
No comments:
Post a Comment