Pages

January 11, 2015

RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI AMBULANCE KITUO CHA AFYA CHALINZE


 Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (katikati) akikabidhi gari jipya la kubebea wagonjwa (Ambulance), kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo,Dk. Mastidia Rutaihwa kwa ajili ya Kituo cha Afya cha Chalinze, katika mkutano wa hadhara uliofanyika mjini Chalinze jioni hii. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni Mganga Mkuu wa kituo hicho, Dk. Bamba Victor na Diwani wa Kata ya Bwilingu, Nasa Karama.
 Muumini wa Dini ya Kikristo, Heema Said akitoa neno la shukrani kwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete (aliyevaa koti kushoto) alipokabidhi ambulance hiyo. Ridhiwani alisema kuwa yeye hivi sasa ni mbunge wa vyama vyote jimbo humo hivyo Ambulance aliyoitoa itoe huduma kwa wakazi wote wa jimbo hilo bila kubagua watu kutokana na itikadi zao. Pia aliuasa uongozi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha wanatunza vizuri gari hilo.

 Dk Rutaihwa akimkabidhi ufunguo wa gari hilo Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya cha Chalinze, Dk.Victor baada Ambulance hiyo kukabidhiwa na Mbunge Ridhiwani.

 Dk. Victor akitoa shukurani kwa Mbunge Ridhiwani kwa msaada huo wa Ambulance

 Wakifurahia kwa pamoja kupata usafiri huo muhimu kwa wagonjwa

 Mbunge Ridhiwani Kikwete na Dk. Rutaihwa wakiangalia ndani ya ambulance hiyo

 Ridhiwani  pamoja na viongozi wa dini ya kiislamu wakiliombea dua gari hilo. Kutoka kulia ni Alhaji  Sheikh Hussein Fuko na Alhajj Khamis Magula

 Ridhiwani (katikati) na Mbuunge wa Jimbo la Mtera, Lusinde wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Kituo cha Afya cha Chalinze akiwemo Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk. Rutaihwa.

 Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo, Dk.Mastidia Rutaihwa akitoa shukurani kwa Ridhiwani kwa msaada wa Ambulance na kuahidi kuitunza

 Ridhiwani akipongezwa na wananchi kwa kuwapatia ambulance

 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Hafsa Kazinja akicheza muziki na mmoja wa wazee wa Chalinze alipotumbuiza katika mkutano huo

 Ridhiwani akihutubia katika mkutano huo

 Sehemu ya umati wa watu waliohudhuria makabidhiano ya Ambulance katika viwanja vya Miembe saba mjini Chalinze
 
(PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...