Kiungo
mshambuliaji wa Borrusia Dortmund Marco Reus huenda akashindwa kutimiza
ndoto yake ya kujiunga na Fc Barcelona baada ya klabu hiyo kushindwa
kwenye rufaa yake ya kupinga adhabu ya kuzuiwa kufanya usajili katika
madirisha mawili yajayo ya usajili .
Dortmund italazimika kumuuza nyota huyo ambaye ana kipengele
kinachomruhusu kuondoka endapo timu yoyote itakuja na dau la euro
milioni 25 , kipengele ambacho kitaweza kutumika baada ya kumalizReus
ambaye inafahamika wazi kuwa ataondoka Dortmund msimu ujao aliwahi
kuiahidi Barcelona kuwa atajiunga na klabu hiyo baada ya kumalizika kwa
msimu huu lakini ahadi hiyo huenda ikashindwa kutimia kwani Barcelona
wako chini ya adhabu ya Fifa ya kutosajili mchezaji yoyote kwa vipindi
viwili vya usajili baada ya kukutwa na hatia ya kukiuka kanuni za
usajili kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 18.
Kitendo cha mahakama ya rufaa za michezo ya CAS iliyoko nchini Uswisi
kuitupilia mbali rufaa ya Barcelona huenda kikaipa Real Madrid faida ya
kuingia na kumsajili mchezaji huyo huku wakifahamu kuwa Barcelona
hawataweza kuhusika kwenye usajili wake .
Marco Reus ataihama Borrusia Dortmund baada ya kumalizika kwa msimu huu .
Madrid kama ilivyo kawaida hasa kwa rais wao Florentino Perez mwenye
kupenda kusajili wachezaji wenye majina makubwa ‘galacticos’ wako kwenye
orodha ndefu ya timu kubwa zinazouvizia usajili wa Reus , orodha
inayojumuisha timu za Manchester City , Manchester United , Arsenal ,
Liverpool Chelsea na Bayern Munich .Kwa hali ilivyo sasa Real Madrid
wanaonekana kuwa na nafasi kubwa ya kumsajili Reus baada ya kuwepo kwa
makubaliano ya mazungumzo ya mdomo baina ya Rais wa Borusia Dortmund
Reinhard Rauball na rais wa Madrid Florentino Perez ambapo rais huyo wa
Dortmund alimuahidi Perez kuwa endapo Reus atawekwa sokoni Madrid
watapewa kipaumbele .
Kitendo cha Barcelona kufungiwa kufanya usajili kwenye vipindi viwili
mfululizo kinaipa Real Madrid fursa ya kumsajili Marco Reus .
Katika hali ya kawaida Bayern Munich wangeweza kuwa na kipaumbele cha
kumsajili nyota huyo wa timu ya taifa ya Ujerumani lakini viongozi wa
Borrusia Dortmund waliapa kuwa hawatamruhusu mchezaji wao mwingine
kujiunga na Bayern Munich baada ya klabu hiyo kuwasajili nyota wawili wa
Dortmund Mario Gotze na Robert Lewandowski katika misimu ya hivi
karibuni .
No comments:
Post a Comment