Mwanafunzi mmoja nchini Kenya amepewa kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kumtukana rais wa Kenya Uhuru Kenyatta katika mtandao.
Alan Wadiu Okengo mwenye umri wa miaka 25 pia atalipa faini ya dola 2,200 la sivyo ahudumie kifungo kingine cha mwaka mmoja.
Alikuwa
ameshtakiwa kwa kutoa matamshi ya chuki baada ya kusema kuwa watu wa
kabila la rais la kikuyu wanafaa kuwekewa mipaka katika maeneo fulani.
Mwanablogu mashuhuri nchini humo pia alishtakiwa baada ya kumwita rais Uhuru Kenyatta 'rais ambaye hajakomaa'.
Kenya ina
mitandao mahiri na mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza amesema kuwa kesi
hiyo imezua mjadala mkubwa kuhusu kile kilichosahihi katika
mitandao.CHANZO:BBC
No comments:
Post a Comment